Afisa uangalizi wa uchaguzi kutoka LHRC HAMIS MKINDI akizungumza na wanahabari mapema leo kuhusu kazi hiyo waliyoifanya na kasorozilizojitokeza katika uchaguzi huo |
Baada
ya kufanya uangalizi kwa njia za kisasa katika uchaguzi wa serikali za mitaa
uliofanyika jumapili nchini Tanzania kituo cha sheria na haki za binadamu nchni
LHRC kimeibuka na kudai kuwa uchaguzi huo ulijawa na kasoro nyingi ambazo
zinafanya uchaguzi huo upoteze uhalali kwa kuwa ulikiuka misingi ya katiba na
haki ya wananchi ya kupiga kura.
Akizungumza
na wanahabari leo afisa muangalizi wa uchaguzi kutoka LHRC wakili HAMIS MKINDI
amesema kuwa kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi huo zimeathiri kwa kiasi
kikubwa zoezi zima la uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wameitaka serikali
kupitia wizara husika ambayo ni ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa na serikali
za mitaa TAMISEM kuwajibika kwa kushindwa kusimamia uchaguzi huo kikamilifu.
Akizitaja kasori
hizo amesema kuwa kushindwa kwa wananchi kupiga kura,kukosekana kwa karatasi
za kupigia kura,kufungwa kwa vituo vya kupigia kura siku ya uchaguzi bila
sababu ya msingi,kukosewa kwa karatasi za kupigiwa kura kukosekana kwa karatasi
za kupigia kura,na pia kukusekana kwa majina ya wapiga kura ni kasoro
ambazo zinaonyesha wazi kuwa zoezi hili lilifanyika bila maandalizi na kwa lugha
nyingine ni kukurupuka.
Aidha
LHRC wamelaani vikali vitendo vya vurugu zilizojitokeza katika maeneo
mbalimbali na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za watu na serikali ambapo
taarifa za waangalizi wa kituo hicho zinaonyesha kuwa vurugu nyingi zilitokana
na udhaifu wa usimamizi na wanachi kuamua kufanya vurugu baada ya kuona mambo
hayaendi kama yalivyotakiwa kwenda.
wabahabari mbalimbali wakisikiliza kwa makini |
Pamoja
na hayo kituo kimewapongea wananchi wote waliojitokeza kwa wingi kutumia haki
yao ya kikatiba katika kupiga kura ambapo wamesemakuwa mwaka huu muamko ni mkubwa hasa kwa vijana hali ambayo inatia matumaini kuwa sasa watanzania wameanza
kutambua haki yao ya kupiga kura
No comments:
Post a Comment