JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM LINATOA
TAHADHARI WAKATI WA UCHAGUZI WA MARUDIO, SERIKALI ZA MITAA.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa
tahadhari kwa wananchi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa wakati
wa zoezi la marudio ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika
tarehe 21/12/2014 katika baadhi ya vituo vya kupigia kura jijini Dar es Salaam.
Awali, uchaguzi huo ulifanyika nchini kote tarehe 14/12/2014 na
kulazimika kuahirishwa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura kutokana na
sababu mbalimbali. Katika mkoa wa Dar es Salaam uchaguzi huo uliahirishwa
katika vituo mbalimbali kama ifuatavyo:
Aidha, Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi huo
unafanyika kwa amani na utulivu kama ulivyopangwa. Kutakuwa na askari waliovaa
sare nadhifu, na askari wa kiraia ambao watakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa
wakati wote amani inatawala katika vituo vya kupigia kura. Askari hawa
watatumia weledi wa hali ya juu ili zoezi hilo liendeshwe kwa utulivu mkubwa
ikizingatiwa vituo ni vichache ikilinganishwa na uchaguzi wa tarehe 14/12/2014.
ONYO:
Wananchi wanatakiwa kutofanya
yafuatayo katika siku ya kupiga kura:
1. Kutofanya kampeni yoyote siku ya kupiga kura.
2. Kutovaa mavazi yanayoonyesha ushabiki kwa chama
chochote cha siasa.
3. Kutovunja sheria yoyote, kanuni, na taratibu
zinazotawala uchaguzi wa serikali za mitaa
4. Kufuata sheria za nchi ikiwemo sheria mama yaani
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
Aidha, yetote atakayekwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu
zilizopo atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kupelekwa
mahakamani.
“UTII WA SHERIA BILA SHURUTI NI MUHIMU KUZINGATIWA WAKATI WOTE”
S. H. KOVA
KAMISHNA WA
POLISI KANDA MAALUM
DAR ES
SALAAM
No comments:
Post a Comment