Mgeni rasmi katika uzinduzi huo katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria MAIMUNA TARISHI pamoja na kaimu mkurugenzi wa WLAC wakizundua report hiyo mapema leo |
Chama cha wanawake wanasheria Tanzania WLAC leo
kimezindua report yake ya hali ya watoto waliopo katika magereza kwa makosa
mbalimbali ya jinai report ambayo inaonyesha bado kuna changamoto mbalimbali
zinazowakuta watoto wanaotumikia adhabu mbalimbali katika magereza huku wadau
wakiombwa kuwatafitia ufumbuzi watoto hao kwani bado ni msaada kwa taifa.
Akisoma mambo kadhaa yanayopatikana katika report hiyo
mwanasheria mkuu wa WLAC ROBERT CHUWA amesema kuwa moja ya changamoto
kubwainayowakumba watoto wanaotumikia adhabu katika magereza yetu ni pamoja na
kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu makosa waliyofanya pamoja na kukosa watu
wa kuwapa elimu hiyo kwa muda muafaka.
Aidha amesema kuwa chanagamito nyingine iliyopo katika
mahakama zetu pamoja na polisi watoto kudanganya umri wao pindi wanapokutwa na
makosa kwa lengo la kuepuka adhabu za watu wazima na kudanganya kuwa wana umri
chini ya miaka 18.
Mgeni rasmi katika
hafla hiyo alikuwa katibu mkuu wizara ya katiba na sheria mh MAIMUNA TARISHI pamoja
na kuwapongeza WLAC pamoja na wadau wengine kwa kutoa msaada wa kisheria kwa
watoto waliopo magerezani amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau
wengine wanaendelea kuwasaidia watoto hao kwa hali na mali kwani wanatambua
fika kuwa watoto hao wanahitaji msaada wa kisheria ili kubadilika na kuwa
katika hali nzuri
mwanasheria mkuu wa WLAC ROBERT CHUWA ambaye ndiye moja ya watu walioandaa report hiyo akitoa machache yaliyopo ndani ya report hiyo |
Awali akizungumza kaim mkurugenzi wa WLAC BI GRACE
DAFA amesema kuwa hapo awali walikuwa hawatoi msaada wa kisheria kwa makosa
yanayowahusu watoto lakini ilipofika mwaka 2000 kwa kushirikiana na shirika la
umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wakaanza kutoa msaada huo wa
kisheria kwa kutumia sharia ya mwaka 2009 ya watoto ambayo ilitaka watoto wenye
makosa wahukumiwe kama watoto na sio watu wazima na ndipo shirika hilo lilianza
rasmi kuwatetea watoto.
Shirika la WLAC lilianza rasmi kufanya kazi zake mnamo
mwaka 1989 nchini Tanzania na hadi sasa limekuwa na mafanikio makubwa kwa kutoa
msaada wa kisheria katika Nyanja mbalimbali
VICTORIA MGONELA ambaye ni mtaalam wa ulinzi na usalama wa mtoto UNICEF ambao wao ndio wadau wakubwa wa WLAC waliofanikisha kupatikana kwa report hiyo akizungumza katika hafla hiyo |
Wadau mbalimbali waliohudururia katika uzinduzi huo |
Kaimu Mkurugenzi wa WLAC BI GRACE DAFA akizungumza katika hafla hiyo. |
No comments:
Post a Comment