Harufu ya kuisha kwa mgogoro baina ya Zitto Kabwe na
chama chake cha Chadema inanukia, lakini mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini
anataka kuwapo na mazungumzo kubaini tatizo ili atakayebainika kuwa
alifanya makosa awe tayari kuomba radhi hadharani.
Zitto alikiri bungeni kuwa amekuwa “akimiss” harakati zilizokuwa
zikifanywa na vyama vya upinzani wakati wa Bunge Maalumu la Katiba,
harakati zilizozaa Umoja wa Katiba ya Wananchi na kufurahia kuhudhuria
kwa mara ya kwanza vikao vya umoja huo.
Zitto, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(PAC), alipata fursa ya kuingia vikao vya Ukawa wakati wapinzani
walipoungana tena kupambana dhidi ya wizi wa fedha kutoka Akaunti ya
Tegeta Escrow, sakata ambalo liliwekwa bayana na kamati yake baada ya
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila kulifikisha bungeni, lakini
hakudokeza lolote kuhusu Chadema.
Hata hivyo, mapema wiki hii, Zitto, ambaye Novemba mwaka jana alivuliwa
nyadhifa zote kwenye chama hicho kwa tuhuma za kukihujumu, lakini
akafanikiwa kulinda uanachama wake baada ya kufungua kesi mahakamani na
kufanikiwa kupata amri ya kuzuia asijadiliwe.
Baada ya kuongoza PAC kuchunguza wa tuhuma za Escrow na kufanikiwa
kulishawishi Bunge kufikia maazimio manane ya kuwashughulikia kisheria
wahusika kwenye uchotwaji huo wa fedha, kumekuwapo na wito kutoka kwa
baadhi ya wafuasi wa Chadema kutaka pande hizo mbili zimalizane.
“Kabla ya jambo lolote kufanyika, ili kukata kiu ya Watanzania wanaotaka
kuona tunaondoa tofauti zetu, ni lazima kusema ukweli na kila upande
kuwa tayari kuomba radhi hadharani pindi ikibainika ulifanya makosa,”
alisema Zitto alipotakiwa kuzungumzia harakati hizo za kumrejesha
Chadema.
“Ukweli wangu ndani ya Chadema ni nini? Lakini mimi ninaona sina kosa
ndani ya Chadema. Ninachotaka mimi nielezwe ukweli bila chembe ya shaka
makosa yangu mimi ni nini,” alisema na kuongeza:
“Nitakuwa tayari kuomba radhi hadharani kama ikibainika nilifanya makosa
na kama ikibainika chama kilifanya makosa, nacho kiwe tayari kuomba
radhi hadharani na ukweli uwe mbele katika maridhiano.
“Kama hakutakuwa na ukweli itakuwa vigumu kupata mwafaka. Mimi sina
tatizo. Nirudie nilivyosema bungeni kuwa nina-miss sana (ninapenda sana
kuwamo kwenye) harakati za mageuzi kipindi hiki za kuiondoa CCM
madarakani.”
Katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kuvuliwa nyadhifa
zote, Zitto alisema: “Natambua kuwa wapo ambao wangependa kutumia nafasi
zao kudhoofisha mapambano ya siasa za demokrasia nchini mwetu. Napenda
wanachama wa Chadema na wapenda demokrasia watambue kuwa, mimi bado ni
mwanachama mwaminifu wa chama hiki.
“Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia.
Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina; waumini
wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu; na wapenda siasa safi dhidi ya
watukuzao siasa majitaka.”
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye binafsi aliguswa na mzozo
huo, hakuwa tayari kuzungumzia kumaliza matatizo baina ya chama na
Zitto.
No comment (sina maoni) kwa hilo. Siwezi kuzungumzia suala hili katika media (vyombo vya habari),” alisema Mbowe
Hoja ya kutaka Zitto arejeshwe Chadema imekuwa ikisambaa katika mitandao
ya kijamii na kwa baadhi ya wanasiasa baada ya kuonekana kuwa karibu na
viongozi wa chama chake wakati Kamati ya PAC ilipoibua ufisadi wa Sh306
bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow wiki iliyopita.
Wakati akihitimisha mjadala wa sakata la Escrow, mbali na kueleza bayana
kuwa alifurahia kuhudhuria vikao vya Ukawa kwa mara ya kwanza, Zitto
alikwenda mbali na kumpongeza “kwa namna ya pekee” Mbowe kwa jinsi
walivyoshirikiana katika sakata hilo.
Zitto alisema hilo lilikuwa ni jambo la kitaifa ndiyo maana wabunge wote wa upinzani bila kujali vyama vyao waliungana.
Alisema mara baada ya sakata hilo kumalizika watu mbalimbali wamekuwa
wakizungumzia kufanyika kwa maridhiano ili awe sehemu ya Ukawa na kwamba
haoni tatizo.
“Katika hili, kipekee namshukuru kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kuniunga mkono katika sakata hili,” alisema Zitto.
Kuhusu taarifa za kujiunga kwake na chama kipya cha ACT-Tanzania alisema: “Hizo ni taarifa ambazo hazina ukweli wowote.”
Kuhusu kesi aliyofungua mahakamani dhidi ya Chadema, Zitto alisema:
“Nilifungua kesi kwa sababu ya kulinda uanachama wangu, lakini
mazungumzo yakifanyika na kujua kosa langu ni nini, nitaifuta kesi hiyo
na kuanza upya harakati.”
Zitto.
Kuhusu taarifa za kujiunga kwake na chama kipya cha ACT-Tanzania alisema, “Hizo ni taarifa ambazo hazina ukweli wowote.”
Kuhusu kesi aliyofungua mahakamani dhidi ya Chadema, Zitto alisema:
“Nilifungua kesi kwa sababu ya kulinda uanachama wangu, lakini
mazungumzo yakifanyika na kujua kosa langu ni nini, nitaifuta kesi hiyo
na kuanza harakati.”
No comments:
Post a Comment