Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki zabinadamu Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya mchakato wa kura ya maoni juu ya katiba pendelezwa |
Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC leo
kimeungana na baadhi ya wanahabarakati wanaotaka mchakato wa kura ya maoni juu
ya katiba inayopendekezwa kuahirishwa mpaka hapo daftari la wapiga kura
litakapokuwa tayari ikiwa ni pamoja na mapungufu mengine yanayojitokeza katika
mchakato huo kurekebishwa.
Akizungumza na wanahabarari asubuhi ya leo
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa kituo
hicho kimekuwa kikifwatilia mchakato huo kwa karibu ikiwa ni pamoja na kusoma sheria
ya kura ya maoni ambapo wamebaini mapungufu mengi na endepo yasipofanyiwa
marekebisho yanaweza kuathiri zoezi zima la kura ya maoni na kuwanyima haki
watanzania wengi kushiriki katika zoezi hilo muhimu kwa Tanzania.
Akitaja mapungufu makubwa ambayo yanaukumba mchakato
huo Bi HELLEN amesema changamoto ya muda bado ni kubwa ambapo kwa mujibu wa sheria
ya kura ya maoni Tume ya Taifa ya uchaguzi inapaswa kuboresha daftari la wapiga
kura ndipo ipigwe lakini hadi leo terehe 23 mwezi huu hadi 28 february ni siku
36 tu na haionyeshi kuwa kuna muda wa kutosha wa kuboresha daftari la kudumu
pamoja na vitambulisho vipya.
Aidha ameyataja meneo
mengine ambayo yana matatizo kuelekea kura hiyo ni uteuzi wa kura ya maoni
,vituo vya kupigia kura ambapo sheria inaelekeza kuwa tume inaweza kutotumia
majimbo ya kawaida na kutengeneza majimbo mapya ambapo amesema kuwa inaweza
kuwa hatari kwani tume inaweza kuvuruga zoezi nzima kwa kutotenga vituo sahihi
kulingana na uuwiano wa watu
Wanahabari wakiwa makini kusikiliza sakata hilo |
Maeneo mengine yenye kasoro ni usajili wa kamati za
kura za maoni,utangazaji wa matokeo ya kura ya maoni,pingamizi la
matokeo,kulipia gharama ya shauri,upigaji kura kwa walio nje ya kituo,pamoja na
swala la rufaa.
Katika hatua nyingine LHRCwameshauri kuwa sheria ya
kura ya maoni ipelekwe tena bungeni ifanyiwe marekebisho hayo ya msingi,pamoja
na serikali kutoa nakala za kutosha za katiba pendekezwa kwa wananchi waweze
kuendelea kuielewa wakati maswala mengine yanaendelea kufanyiwa kazi.
UKITAKA KUSOMA TAMKO LAO BONYEZA CHINI HAPO MDAU
No comments:
Post a Comment