Pichani ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini TFDA Bwana Mitangu Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar Es Salaam |
NA
KAROLI VINSENT
MAMLAKA
ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imezifutia Usajili na kuzuia Uingizaji Dawa
tano za Binadamu kutokana na kuwepo makosa mbalimbali.
Hayo yametangazwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka
ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Mitangu Adam Fimbo Wakati wa Mkutano na
Waandishi wa Habari ambapo alisema Mamlaka hiyo katika kupitia mifumo ya
ufuatiliaji wa usalama na ubora wa dawa nchini wamebaini uwepo wa dawa
duni kwenye soko zenye madhara na zisizofaa kwa matumizi ya Binadamu.
Ambapo katika kufuatilia huko,Mamlaka hiyo imefikia hatua ya kufuta
usajili wa aina tano za dawa za binadamu ,ambazo ni Dawa ya kutibu
“Fungus” ya vidonge na kapsuli aina ya ketocanazole ambayo mamlaka hiyo imesema
sababu ya kuzuia kwake ni kutokana na kubaini dawa hiyo inasababisha madhara
hatarishi katika Ini kwa watumiaji.
Na nyingene ni dawa ya kutibu malaria ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine
nayo pia Mamlaka hiyo imesema sababu ya kufutia usajili na kuzuia kuingia
nchini kutokana na mabadiliko ya mwongozo wa kisera wa kupima na kutibu malaria
wa mwaka 2013 wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ambapo mabadiliko hayo
yamebaini Amodiaquine ikitumika peke yake inaleta usugu wa vimelea vya malaria.
Mkurugenzi huyo aliitaja dawa nyingine Dawa ambayo ni hatari kwa binadamu ni
Dawa ya kutibu mafua na kikohozi za Maji,Vidonge na kapsuli zenye
kiambato hai aina ya Phenylpropanol amine ambacho anasema kinaleta madhara
hatarishi kwa binadamu kama vile kiharusi (Hemorrhagic sroke).
Mbali na hizo Dawa zengine ni Dawa ya kuua bacteria ya Sindano aina ya
Chloramphenic ol Sodiam Succinate inayotengenezwa nchini India pamoja na dawa
ya kuua Bakteria ya Maji na kapsuli aina ya Cloxacillin ambazo zote kwa pamoja
bwana Fimbo alizitaja kwamba zina madhara kwa watumiaji ikiwemo kushindwa
kupumua na kupoteza Fahamu.
Katika Hatua Nyingine mamlaka hiyo imebadili na kudhibiti aina nne ya dawa
mbalimbali.
Dawa hizo ni Dawa ya kutibu imebadilika matumizi yake,malaria ya vidonge yenye
mchanganyiko wa Sulphadoxine na pyrimethamine na dawa aina ya Kanamycin
Amikacin na Levofloxian.
No comments:
Post a Comment