NA SULEMAN MAGALI
Kanisa la Anglikana Dayosisi ya
Dar es salaam, linatarajia kuazimisha miaka hamsini ya utumishi wake mapema
jumapili ambapo askofu wake mkuu wa dayosisi hiyo ametumia fursa hiyo
kuwataka waumini wa kanisa hilo kujitokeza kwa wingi kwenda kuanzimisha
miaka hiyo hiyo jumapili,
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema hii leo katika makao makuu ya dayosisi
hiyo yaliyoko Ilala kona ya Arusha na Moshi, Mokiwa amesema kuazimisha
miaka hamsini hiyo ni faraja kwa kanisa kwani katika miaka hiyo 50
kunachangamoto mbalimbali ambazo kanisalimepitia
Askofu Valentine Mokiwa ametaja baadhi
ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na kuhudumia jamii katika mazingira
magumu hususani katika sekta ya afya ambayo mpaka sasa wanajitahidi
kuhakikisha kuwa wanajenga vituo vingi kadri wanavyoweza ili kuleta
huduma bora kwa waumini wao na jamii ya kitanzania kwa ujumla,
Aidha akizungumzai maadhimisho hayo ya
miaka 50 ya dayosisi ya Dar es salaam, Mokiwa amesema maadhimisho hayo
yataenda sambamba na makongamano mbalimbali ya vijana, michezo
mbalimbali ikiwemo mpira wa wavu, basketi ball, na michezo mingine,
Aidha akizungumzia maadhimisho hayo kwa
undani zaidi, Mokiwa amesema, maadhimisho hayo yatawaleta waumini wa
kanisa hilo karibu na viongozi na hivyo kuondoa ile dhana ya
kuchangamana kati ya viongozi na waumini wao,
Aidha Askofu mokiwa ametaja baadhi ya
mafanikio ambayo dayosisi hiyo wameyapata katika kipindi hicho cha miaka
50, na kusema kuwa wamefanikiwa kuwa na vitega uchumi mbalimbali
ikiwemo shule mbalimbali za nusery, za msingi.
Amesema, katika mikakati yao ambayo
wameipanga ni kuanza kuwa na kinywa cha kanisa ambapo wamesema kanisa
lifungua kituo cha redio ili waumini wake waweze kupata taarifa sahihi
za kanisa kupitia chombo chao,
Na katika kuhakikisha kuwa dhamira yao
hiyo nzuri inafikiwa, kanisa limeamua kuchangisha fedha kupitia taasisi
mbalimbali kama vile za sumatra na zinginezo ili kuwa na fedha za
kuanzisha kituo hicho
No comments:
Post a Comment