Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokelewa na uongozi wa Wizara hiyo mapema leo asubuhi. Mhe. Simbachawene amesisitiza umuhimu wa sekta za nishati na madini kama mhimili mkuu wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuomba ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta za nishati na madini. |
NA KAROLI
VINSENT
WAZIRI mpya
wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Mandeleo na Makazi,Wiliam Lukuvi ameanza kazi
rasmi na kusema hatumuongopa mtumishi yeyote katika wizara hiyo atakayekwenda
kinyume na taratibu,basi hatosita kumtimua kazi.
Kauli ya
Waziri lukuvi ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akitamburishwa
kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na maendeleo na Makazi baada ya
kuteuliwa kwake ambapo alisema anafahamu wizara hiyo imejaa watu wezi,ambao
hawako tayari kumsaidia mtanzania.
“Naingia
hapa najua kuna watu wanafanya dhuruma kwa watanzania na mabosi wao ni matajiri
watu wenye fedha ambao wamegeuza wizara hii kumkandamizia mtanzania na
kumnyonya kutokana na matakwa ya matajiri ambao wanawapa fedha”
“Nataka
niwambie kabisa waondoke kabisa mapema kabla sijawafukuza na kuwapelekea mahakamani,maana
sitomfumbia macho mtu yeyote na wala sitomuogopa”alisema Waziri Lukuvi.
Waziri
lukuvi aliongeza kuwa tatizo la migogoro ya Ardhi,katika wizara hiyo limekuwa
kubwa sana na kusema atapambana nalo na kuhakisha anatatua tatizo hilo.
“Kwanza
najua wananchi wa hapa mkoa wa Dar es Salaam,wamesaidiwa sana na Wizara
hii,nataka niwambia naingia katika wizara hii,nitakuwa natumia mda mwingi
kufanya kazi za mikoani”alisema Waziri Lukuvi.
Kauli hiyo
ya Waziri lukuvi imekuja siku moja kupita baada Rais Jakaya Kikwete kumteua
kuwa Waziri kwenye Wizara hiyo,ambapo imetokana na Kujiuzulu kwa Profesa Anne
Tibaijuka kutokana na kuingiziwa Bilioni 1.6 na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP
Engineering Bwana James Rugimalira.
Kwa upande
wake Naibu Waziri mpya wa Wizara hiyo, Angellah Kairuki akawataka
wafanyakazi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuacha uvivu na kusema
atawashugulikia watumishi wazembe.
Naye Katibu mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo na makazi Bwana Alphayo J. Kidata akizungumza kwa niaba ya Wafanyakazi
alimkaribisha Waziri lukuvi na kuwasihi wafanyakazi wenzake wampe ushirikiano.
MRITHI wa Muongo aliyasema haya
Waziri wa
Nishati na Madini ,George Simbachawene amesema kuwa watanzania wamuamini
ataendeleza kwa kasi ile ile katika kuwafikishia wananchi maendeleo kupitia
sekta za nishati na madini.
Hayo ameyasema
leo wakati alipoanza kazi rasmi katika Wizara hiyo akichukua nafasi ya Profesa
Sospeter Muhogo aliyejiuzulu wiki iliyopita,amesema kila mtu sio mkamilifu hata
mitume watu wengine hawakumuamini.
Simbachawene amesema ana uzoefu wa kufanya kazi na kuachana na vyeti kwani vyeti ni ziada lakini kalama ya uongozi ndiyo inayohitajika.
Simbachawene amesema ana uzoefu wa kufanya kazi na kuachana na vyeti kwani vyeti ni ziada lakini kalama ya uongozi ndiyo inayohitajika.
Sehemu
ya waandishi wa hab-ari wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini,Mhe.
George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza nao leo
Aidha amesema wanaotilia shaka uteuzi wake watakuwa na kigezo lakini kila mtu hawezi kuamini kila binadamu ana mapungufu kwa namna anavyoona mtu.
Aidha amesema wanaotilia shaka uteuzi wake watakuwa na kigezo lakini kila mtu hawezi kuamini kila binadamu ana mapungufu kwa namna anavyoona mtu.
Simbachawene amesema atafuatilia
usiri wa mikataba lakini sasa anasoma mazingira kwanza na kuweza kuweka bayana
suala hilo.
“Niko hapa watu waniamini kutokana
na kazi zangu na watanzania waniamini niweze kufanya kazi niliyoaminiwa kwa
niaba ya watanzania wenzangu”amesema Simbachawene
No comments:
Post a Comment