Mwenyekiti wa tume hiyo ,Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizngumza na wanahabari mapema leo juu ya zoezi hilo |
Tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania NEC imesema kuwa
sasa Tanzania inaweza kutumia mfumo mpya wa uandikishwaji wa daftari la kudumu
la wapiga kura wa BVR kutokana na mfumo huo kuonyesha mafanikio makubwa baada
ya kuufanyia majaribio katika maeneo kadhaa nchini.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam
mwenyekiti wa tume hiyo ,Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa tume hiyo
ilifanya majaribio ya kutumia mfumo huo mpya wa uandikishwaji katika majimbo
matatu ambayo ni KAWE,KILOMBERO NA KATAVI ambapo mfumo huo ulionyesha kufanya kazi kwa
uhakika na kujiridhisha kuweza kuutumia katika zoezi la nchi nzima mapema mwaka
huu.
“Tunasema kuwa tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa
sababu matokeo ya jumla yanaonyesha kuwa idadi ya wapiga kura waliojitokeza
kujiandikisha ilikuwa kubwa na kuvuka malengo waliyokadiriwa kuandikishwa”amesema
lubuva
Katika takwimu zinaonyesha kuwa kwa mkoa wa dar es
salaam kata ya bunju wapiga kura 15,123 waliandikishwa kati ya 27,148 na kata
ya mbweni wapiga kura 6200 walianndikishwa kati ya 8278,mkoa wa morogoro kata
ya ifakara kakingiuka ipangala,na viuwanja sitini wapiga kura walioandikishwa
ni 19,188 wakati makisio yalikiuwa watu 17,790 na mkoa wa katavi halmashauri ya
milele kata ya ikuba,usevya na kibaoni wapiga kura walikuwa 11,210
walioandikishwa wakati makisio yaklikuwa
watu 11,394 ambapo amesema kuwa
matokjeo hayo yanaonyesha ni jinsi gani wananchi wamekuwa na muamko wa kutumia
mfumo huo na vifaa hivyo vilifanya kazi vizuri.
Aidha jaji LUBUVA amesema kuwa zoezi hilo kwa nchi
nzima litaanza mapema kwani daftari hilo ndilo litakalotumika katika kuipigia
kura katiba mpya katika kura ya maoni pamoja na uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka
huu.
Pamoja na hayo jaji LUBUVA amewataka watanzania
kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo pindi lityaka[poanza nchi nzima kwa
lengo la kujiandikisha katika daftari hilo kwani litawasaidia katika kuipigia
kura katiba mpya na uchaguzi mkuu ujao.
TAARIFA YOTE YA TUME IKO HAPA-----
TAARIFA YOTE YA TUME IKO HAPA-----
Ndugu Waandishi wa Habari,
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Watendaji wa Tume,
Mabibi na Mabwana.
Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisheni kwa mara nyingine
katika Mkutano huu. Nawashukuru kwamba, pamoja na majukumu mengi mliyo
nayo, mmeweza kuupa umuhimu wa pekee mkutano wetu huu na kuhudhuria kwa
wingi. Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, nasema Ahsanteni na
Karibuni sana.
Katika mkutano huu, Tume inalenga
kutoa taarifa kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi la majaribio ya
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (Pilot Registration) kwa
mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) zoezi ambalo lilikamilika
wiki iliyopita.
Ndugu Wanahabari,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imepewa jukumu la kisheria
Kuandikisha Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na
kuliboresha Daftari hilo kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani. Kwa mujibu wa Sheria ya Kura
ya Maoni, Daftari hili la Kudumu pia litatumika katika Kura ya Maoni
kuhusu Katiba Inayopendekezwa.
Ndugu Wanahabari; mtakumbuka kuwa,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa katika mchakato wa Maandalizi ya
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia
Mpya ya ”Biometric Voter Registration” (BVR) na mara kwa mara imekuwa
ikiomba kukutana nanyi ili kuwapa taarifa kuhusu hatua mbalimbali ambazo
Tume imekuwa ikizipitia.
Kwa kuwa Uboreshaji huu ulihusisha
matumizi ya vifaa vya teknolojia ya kisasa, vifaa ambavyo vilikuwa
havijawahi kutumika katika Uboreshaji nchini, tuliona si vyema kuagiza
vifaa vingi kabla ya kuvifanyia majaribio. Zoezi la majaribio
lilifanyika ili kuwa na uhakika kuwa vifaa hivi vya Biometric
Registration vina uwezo wa kuandikisha Wapiga Kura katika mazingira ya
nchi yetu. Zoezi hili liliangalia uwezo wa watendaji kutumia BVR katika
uandikishaji na pia uwezo wa vyombo vyenyewe katika Software na Hardware
kwenye uandikishaji. Katika zoezi hili tuliangalia changamoto
zilizojitokeza ili kuzipatia ufumbuzi kabla ya kuanza Zoezi halisi la
Uandikishaji wa nchi nzima.
Ndugu Wanahabari,
Kama nilivyosema, Tume inakutana nanyi ili kuwapa taarifa kuhusu
Tathmini ya Utekelezaji wa zoezi la Majaribio la Uboreshaji wa Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura lililofanyika kwa siku saba (7) katika Kata za
Bunju na Mbweni katika Jimbo la Kawe, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar
es salaam; Kata za Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja
Sitini katika Jimbo la Kilombero Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero,
mkoani Morogoro; na Kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni katika Jimbo la
Katavi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Tume kwa namna ya pekee,
inawashukuru sana Waandishi wa Habari kwa kujitokeza na kufuatilia zoezi
hili la majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Waandishi wa Habari wamesaidia sana katika kuhamasisha Wananchi wa
Majimbo husika kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura. Vilevile, Waandishi wa Habari wamesidia katika
kutoa taarifa za maendeleo ya zoezi hili kitu ambacho kimesaidia
kufanikisha zoezi hili.
Jumla ya BVR Kits 250 zilitumika
katika Uboreshaji huo kwa mgawanyo ufuatao:- Halmashauri ya Kilombero
BVR Kits 80, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele BVR Kits 80 na Halmashauri
ya Manispaa ya Kinondoni BVR Kits 90. Vituo katika Kata zote vilikuwa
vinafunguliwa saa 2.00 asubuhi na kufungwa saa 12.00 jioni.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Tume inapenda kuwafahamisha kuwa zoezi hilo la Majaribio ya
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika majimbo matatu
yaliyotajwa limefanyika na kukamilika kwa mafanikio makubwa. Changamoto
zilizojitokeza hapa na pale zimetusaidia kupata ufumbuzi ambao
utatusaidia wakati wa Uandikishaji wenyewe nchi nzima.
Tunasema mafanikio makubwa kwa
sababu matokeo ya jumla yanaonyesha kuwa idadi ya wapiga kura
waliojitokeza kujiandikisha ilikuwa kubwa na kuvuka malengo ya
waliokadiriwa kuandikishwa.
Mkoa wa Dar es salaam, Kata za
Bunju Wapiga Kura 15,123 waliandikishwa kati ya 27,148 na Kata ya Mbweni
Wapiga Kura 6,200 waliandikishwa kati ya 8,278. Takwimu hizi za
waliondikishwa inatokana na makisio ya watu tuliyokuwa tumejiwekea
kutokana na matokeo ya sensa mwaka 2012. Mkoa wa Morogoro Kata za
Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja Sitini Wapiga Kura
walioandikishwa ni 19,188 wakati makisio yalikuwa watu 17,790 na Mkoa wa
Katavi Halmashauri ya Mlele kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni Wapiga
Kura 11,210 waliandikishwa wakati makisio yalikuwa watu 11,394. Matokeo
haya yanadhihirisha kuwa vifaa vya uandikishaji vilifanya kazi vizuri na
hivyo vinaweza kutumika katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura kwa nchi nzima.
Pamoja na mafanikio hayo, kama
ilivyo kawaida katika majaribio yoyote kwani ndiyo lengo la kufanya
majaribio, zilikuwepo changamoto kadhaa wakati wa utekelezaji wa zoezi
hilo. Changamoto hizo zinaweza kuwekwa katika makundi makubwa matano
kama ifuatavyo:-
i. Matatizo yaliyotokana na ’Settings’ za BVR Kits;
• Baadhi ya ”BVR Kits” zilitumia camera iliyo katika Laptop badala ya camera iliyowekwa kwa ajili ya kupiga picha.
• Uchukuaji wa alama za vidole (Automatic Process settings) ilisababisha Mfumo kusimama (Crash).
• Tatizo la kuchukua picha iwapo viwango vya ICAO vya ubora wa Picha havijafikiwa kama
• Unrecognise face,
• Unrecognise eye,
• Stretch photo,
• Un even light.
• Uwepo wa Majina yenye ”apostrophe”.
ii. Matatizo yaliyosababishwa na Software;
• Fingeprint Scanner kusababisha Mfumo wa Uandikishaji kusimama (Crash) kutokana na SDK na za vifaa finger print scanner.
• Kuharibika kwa baadhi ya file (File Corruption) kutokana na d11 ya finger print scanner.
iii. Matatizo ya hardware;
• Komputa (Laptop) Kupata Joto kutokana na Bati liliwekwa kuzuia
kuibiwa Laptop kwa urahisi ambapo mahitaji kuwezesha mzunguko wa hewa
ndani ya ”BVR Kit”.
• FlashDrive ya pili (Drive G) kutoonekana hivyo kuhitaji kubadilishwa na kuwa SD card.
• Uharaka wa uchukuaji alama za vidole ambapo ilibidi kufanya mabadiliko.
iv. Matatizo ya lojistiki na matatizo ya Watendaji wa zoezi la Uandikishaji.
• ”BVR Kit” kuchelewa kufikishwa katika Vituo.
• Vurugu wakati wa uandikishaji ambao unahitaji Ulinzi kuwepo.
• Baadhi ya ”BVR Operator” kutokuwa na uwezo au kuwa makini
katika utumiaji wa ”BVR Kits” hivyo kuhitaji elimu zaidi kwa ”BVR Kit
Operator”.
• ”BVR Kit Operator” kubadili Kits kwa tatizo dogo linaloweza kutatulika kwa urahisi.
• ”BVR Kit Operators” kutokuwa na uelewa wa matumizi ya ”Solar
Panel” kwani baadhi ziliwekwa chini ya mti au kutogeuzwa kadri muda
ulivyokuwa unakwenda.
Mbali ya changamoto hizo zilikuwepo pia changamoto nyingine za
kimiundombinu na kibinadamu. Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na
Hali ya Hewa hususan katika jiji la Dar es salaam na Morogoro.
Mtakubaliana nami kuwa pamoja na kuwa jiji la Dar es salaam kwa kawaida
lina hali ya hewa ya joto lakini kwa takribani mwezi mmoja hivi uliopita
kumekuwa na ongezeko la joto hali iliyosababisha hata baadhi ya vifaa
vya kuandikishia hususan ’BVR Kits’ wakati mwingine kushindwa kufanya
kazi inavyotakiwa na hivyo kusababisha shughuli za uchapishaji wa Kadi
za Kupigia Kura kuchelewa.
Aidha, ushirikiano mdogo kutoka kwa Wananchi nao ulikuwa
changamoto iliyosababisha zoezi hilo kwenda taratibu. Baadhi ya wananchi
kushindwa kuzingatia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na BVR Kit
Operators kutokana na uelewa duni kwani ilibainika pia kuwa bado kuna
idadi kubwa ya wasiojua Kusoma na Kuandika. Hali hiyo ilifanya zoezi la
Uchukuaji wa alama za Vidole (Fingerprint) na Utiaji wa Saini kuwa
mgumu.
Kadhalika kumekuwepo na mwamko
mkubwa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha. Hivyo,
kulikuwepo na watu wengi sana katika vituo vya Uboreshaji wa Daftari
hilo la Kudumu la Wapiga Kura. Changamoto zote zilizojitokeza kuhusiana
na settings tuliweza kwa ushirikiano na watengenezaji wa vifaa hivyo,
kuzipatia suluhisho wakati zoezi linaendelea. Pia chanagamoto za
’software’ nazo zimekwishapatiwa suluhisho. Changamoto kuhusu hardware
zitarekebishwa wakati wa utengenezaji wa BVR Kits 7,750 ambazo zilikuwa
hazijaanza kutengenezwa kusubiri matokeo ya zoezi hili la majaribio.
Marekebisho hayo ya hardware pia yatafanywa katika BVR Kits 250
zilizoletwa kwa ajili ya majaribio. Changamoto kuhusu fedha na lojistiki
zinaendelea kushughulikiwa kwa ushirikiano na Serikali. Kuhusu
changamoto za Watendaji tunaendelea kuzishughulikia kwa kuhakikisha
Watendaji tutakaowatumia wanakuwa na utaalam unaotakiwa kuziendesha BVR
Kits hizo.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Napenda pia niongelee baadhi ya masuala yanayohusu zoezi la
Uboreshaji wa Majaribio kwa ujumla. Kwanza ni vyema ieleweke wazi kuwa
kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kwa ajili ya Kura ya Maoni
ya Katiba Mpya, Mpiga Kura atatumia Kitambulisho cha Mpiga Kura
alichopatiwa na Tume baada ya kuandikishwa katika mfumo huu tu na si
vinginevyo. Vitambulisho vilivyotolewa katika uboreshaji huu wa
majaribio ni vitambulisho halisi hivyo kila aliyejiandikisha katika
zoezi hili la majaribio ni muhimu atunze kadi yake kwa ajili ya matumizi
yaliyotajwa kwa kuwa taarifa zake tayari zimeingia katika Kanzi data ya
Tume hivyo hataweza tena kujiandikisha kwa mara nyingine hata kama
atabadilisha kituo cha kujiandikishia.
Ndugu Wanahabari,
Pili, ni muhimu wananchi wakapata taarifa hizi kwa usahihi kwa
vile wapo baadhi ya Watu wanaodhani kuwa kwa kuwa hilo lilikuwa ni zoezi
la majaribio basi watakuwa na fursa nyingine ya kujiandikisha wakati wa
zoezi la nchi nzima. Napenda nisisitize hapa kuwa kwa yeyote
aliyejiandikisha katika zoezi hili, hatatakiwa tena kujiandikisha labda
tu kwa yule ambaye atahitaji kubadilisha taarifa zake kutokana na sababu
kama zilivyofafanuliwa na Tume.
Ndugu Wanahabari.
Napenda nisisitize pia kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inayo
dhamira ya dhati ya kukuza demokrasia kwa kuandaa na kuendesha chaguzi
zake katika mazingira rafiki na wazi yatakayotoa fursa kwa kila raia wa
Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 kutumia haki yake ya kikatiba ya
kuchagua viongozi wake. Tume itakuwa tayari kupokea maoni na ushauri
kutoka kwa wadau mbalimbali
No comments:
Post a Comment