JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO HABARI KUHUSU VIKAO
VYA KAMATI ZA BUNGE KUANZA TAREHE 13 – 23 JANUARI 2015
YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO HABARI KUHUSU VIKAO
VYA KAMATI ZA BUNGE KUANZA TAREHE 13 – 23 JANUARI 2015
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawatangazia Waheshimiwa
Wabunge wote, wadau na umma kwa ujumla kuwa Kamati za Kudumu za Bunge zitaanza
vikao vyake tarehe 13 hadi 23 Januari 2015. Vikao hivyo vitakavyoutangulia
mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge la Kumi vitajadili na kuchambua pamoja na
mambo mengine Miswada mbalimbali ya sheria.
Miswada itakayopitiwa na
chambuliwa (pamoja na kamati husuka kwenye mabano) ni hii ifuatayo:
i. Muswada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji wa Mwaka 2014 [The Immigration (Amendment) Bill, 2014], [Kamati ya Mambo ya Nje]
ii.
Muswada wa Sheria ya Tume
ya Kudhibiti UKIMWI wa Mwaka 2014 [The
Tanzania Commision for AIDS (Amendment) Bill, 2014, [Kamati ya Masuala ya UKIMWI]
iii.
Muswada wa Sheria ya
Kudhibiti Silaha wa Mwaka 2014 [The
Firearms and Ammunition Control Bill,
2014], [Kamati ya Ulinzi na Usalama]
iv.
Muswada wa Sheria ya
Usimamizi wa Maafa wa Mwaka 2014 [The Disaster Management Bill, 2014], [Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala]
v.
Muswada wa Sheria ya
Udhibiti wa Ajira za Wageni wa Mwaka 2014 [The
Non-Citizen Employment Regulation Bill, 2014], [Kamati ya Maendeleo ya Jamii]
vi.
Muswada wa Sheria ya
Wataalam wa Kemia wa Mwaka 2014 [The
Chemist Professionals Bill, 2014],
[Kamati ya Huduma za Jamii]
vii.
Muswada wa Sheria ya
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2014 [The Government Chemistry Laboratory Bill, 2014], [Kamati ya Huduma za Jamii]
viii.
Muswada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria ya Stakabadhi Ghalani wa Mwaka 2014 [The Warehouse Receipts (Amendment) Bill, 2014, [Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara]. Angalizo: Wakati wa
uchambuzi Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara itashirikiana na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.
ix.
Muswada wa Sheria ya
Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya wa Mwaka 2014 [The Drug Control and Enforcement Bill, 2014], [Kamati ya Masuala ya UKIMWI]
x.
Muswada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2014 [The Written Laws (Miscelaneous Amendments) Bill, 2014, [Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala].
Angalizo: Aidha inashauriwa wakati wa kuchambua Muswada huu Kamati za
kisekta zishirikishwe kwenye kutoa maoni
kwenye marekebisho ya sheria ya sekta husika.
xi.
Muswada wa Sheria ya
Bajeti wa Mwaka 2014 [The Budget Bill,
2014], [Kamati ya Bajeti]
Aidha, kwa taarifa hili Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania wanaombwa kuwasili Jijini Dar es Salaam tarehe 12
Januari 2015 tayari kwa kuanza kazi tarehe 13 Januari 2015.
Imetolewa na Ofisi ya
Bunge,
Idara ya Habri, Elimu kwa
Umma na
Uhusiano wa Kimataifa
07 Januari, 2015
No comments:
Post a Comment