Baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na waandishi wa habari waliohudhuria
uzinduzi huo.
Vodacom imezindua promosheni kubwa kuliko zote
katika historia ya michezo ya bahati nasibu nchini Tanzania ambapo wateja
watajishindia pesa taslimu Sh. bilioni 30/- katika zawadi ndani ya kipindi cha
siku 100.
Akizungumza na waandishi wa habari jjijini leo ,Mtendaji
Mkuu wa
Vodacom Tanzania Rene Meza amesema promosheni hii inajulikana kama JayMillions na inawahusisha wateja wote
wa Vodacom na ni ya kwanza ya aina yake kwani, “kiasi kikubwa cha fedha
kitatolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki.”
Vodacom itatoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-,
washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi mia moja wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku
mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye
thamani ya Sh. 1000/- kila siku.
Meza ameongeza kuwa hii inadhihirisha dhamira ya
kampuni ambayo mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wake pia ina dhamira ya
kubadilisha maisha ya wateja kuwa murua zaidi “ambao wamekuwa wakiendelea
kujiunga na familia ya Vodacom kila siku.”
Kwa upande wake, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko
wa Vodacom, Kelvin Twissa amesema ili kushiriki katika promosheni hii, mteja
yeyote wa Vodacom, aliyeko popote nchini anahitaji kutuma SMS moja tu yenye
neno “JAY” kwenda namba 15544 kila siku ili kujua kama
ameshinda au la. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi
utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa
hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku
inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu.
“”Tofauti na promosheni zilizopita, JayMillions
ni rahisi sana
kushiriki. Tuma ujumbe mfupi mmoja tu na mara moja tu kila siku. Hakuna
maswali mengi, wala chemsha bongo na hivyo kufanya hii kuwa promosheni inayotoa
nafasi kwa wateja wengi kuibuka washindi. Cha muhimu ni kuhakikisha kila siku
unatuma ujumbe mfupi,” alieleza Twissa.
Alisema kila siku namba
zilizoshinda zitapatikana kupitia mfumo mahsusi wa promosheni hii. “Ili kujua
kama namba ya mteja imechaguliwa, tunapenda kukusisitizia mteja wetu kutuma
ujumbe mfupi wa “JAY” kila siku kwenda 15544 ili wasipoteze bahati zao iwapo
namba zao zitakuwa zimechaguliwa. Bila kufanya hivyo, wanaweza kupoteza
mamilioni kwani hawatoweza kujua kama namba zao zilichaguliwa kama washindi
ambapo zinachaguliwa kila siku,” alisisitiza Twissa.
Mwisho
Kuhusu Vodacom Tanzania
Kampuni ya Vodacom Tanzania ni kampuni inayoongozwa
kwa kuwa na mtandao mkubwa na huduma za mawasiliano nchini. Ilianza kutoa
huduma nchini mnamo mwaka 2000, ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) ya
Afrika ya Kusini ambayo pia ni kampuni tanzu ya
Vodafone Group UK.Vodacom Tanzania Limited hisa zake zinamilikiwa kwa
pamoja na makampuni ya Vodacom Group (Pty) na Mirambo Ltd.
Vodacom inaongoza katika soko na kutoa huduma bora
za mawasiliano nchini, na imekuwa mstari wa mbele kubuni huduma bora za
mawasiliano za kuwarahisishia wateje wake maisha. Moja ya huduma inayotolewa na
Vodacom ambayo imeleta mabadiliko makubwa nchini ni M-PESA ambayo hadi sasa
inatumiwa na wateja zaidi ya milioni 5.2. Zaidi ya taasisi 200 nchini zinapokea
malipo kupitia M-PESA. Huduma hii ni suluhisho katika kufanya malipo kwa kuwa
utumiaji wake hauhitaji mpaka uwe na
akaunti ya benki. Hapo ndipo umuhimu wa huduma hii unaonekana kwakuwa idadi
kubwa ya watanzania hawana sifa za kufungua akaunti za benki na idadi ya wenye
akaunti ni wachache. Kwa kupitia M-PESA, mteja wa Vodacom anaweza kuweka akiba
inayofikia milioni 5 katika simu yake, anaweza kutuma, kupokea fedha na kutoa
fedha kutoka kwa mtandao wa mawakala wanaotoa huduma hiyo ambao wameenea nchini
kote. Mteja pia anaweza kuangalia salio
la akaunti yake ya benki akiwa nyumbani.
|
No comments:
Post a Comment