Mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC ndugu HAROLD SUNGUSIA akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam juu ya siku ya kupinga ukeketaji duniani |
NA EXAUD MTEI
Ikiwa leo ni siku ya kupinga vitendo vya ukeketaji duniani imeelezwa kuwa bado mapambano dhidi ya ukatili huo hapa nchini
kwetu Tanzania yanahitaji nguvu ya ziada kwani bado baadhi ya mikoa imekuwa
sugu katika vitendo hivyo ambapo serikali imetakiwa kuchakua hatua mara moja
juu ya watu ambao wanahusika katika vitendo hivyo.
Akizungumza na wanahabari leo mwanasheria kutoka
kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC akiwakilisha mashirika zaidi ya 15
yanayohusika na ukeketaji nchini Tanzania wakili HAROLD SUNGUSIA amesema kuwa
mwaka 2014 umeshughudia watoto wengi wakikeketa, pamoja na jitihada za
kutokomeza vitendo hivyo ambapo ametolea mfano wilaya ya tarime pekee takribani
watoto 1400 walikeketwa na watoto hao ni kutoka katika koo za bukira watoto
212,bukenye watoto 230,iregi watoto 800,pamoja na nyabasi watoto 160,ambapo ni
idadi kubwa sana na ikizingatiwa kuwa ni wilaya moja tu.
IMELDA URIO ambaye ni mkurugenzi wa uwajibikaji na uwezeshaji kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC akizungumza na wnahabari |
Amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa sheria
zinazolikemea tatizo hilo bado cha kusikitisha ni kuwa mila hii imekuwa
ikitekelezwa kwa kasi sana katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania katika
baadhi ya jamii zetu.
“tunaitaka serikali kwa kupitia jeshi la polisi
kusimamia sheria na kuwachuklia hatua za kisheria watu wote watakaobainika
kufanya vitendo hivi”amesema SUNGUSIA
Ameongea kuwa
ukeketaji ni kosa la jinai, na kosa la jinai huwa haliishii yani halina ukomo
wa muda hivyo wanatarajia kuwa kama serikali inamaanisha kweli kupinga
ukeketaji huo basi iweze kufwatilia huko vijijini na kuwabaini wale wote
wanaoshiriki kukeketa watoto na kuwachukulia hatua stahiki
Mwakilishi kutoka chama cha wanahabari wnawake tanania TAMWA bi GOGFUDA JOLA akizngumzia kuhusu shirika lao linavyoshgulikia tatizo la ukeketaji katika maeneo mbalimbali nchini |
Wasaka habari wakiwa wanasikiliza kwa makini |
Aidha mashirika hayo yanayotetea na kupinga vitendo
vya ukeketaji wamewaomba wadau wengine na watanzania kwa ujumla kujiuga kwa
pamoja kupinga vitendo hivyo kwani ni vitendo vya kikatiki kwa mtoto wa kike na
ni kumnyima haki zake za msingi kama mwanadamu,ikiwa ni pamoja na kutoa elimu
zaidi juu ya madhara ya ukatili huo.
Baadhi ya mashirika ambayo leo wameungana kwa pamoja
kupinga vitendo hivyo ni TAWLA,TAMWA,DIAC,CCT,WORD
VISSION,NAFGEM,AFNET,WOWAP,CDF,WLAC,TGNP MTANDAO,WILDAF,BAKWATA,TGNP pamoja na
HOUSE OF PEACE.
TAMKO NZIMA LIKO CHINI
No comments:
Post a Comment