NA EXAUD MTEI
Wadau mbalimbali wa maswala ya usafirishaji,uchukuzi na watanzania kwa ujumla wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kusaidia kuchangia katika mkutano ulioandaliwa na CILT (the charted institute of logistics and transport) mkutano ambao unatarajiwa kufanyika kuanzia terehe 4 mwezi wa tatu hadi tarehe 6 katika hoteli ya mount meru mkoani Arusha.
Akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya maandalizi
ya mkutano huo wa kimataifa makamu mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya
mkutano huo Bregedier HARISON JOSEPH MASEBO amesema kuwa mkutano huo
utawakutanisha magwiji wa maswala ya usafirishaji na uchukuzi kutoka katika
nchi mbalimbali barani Africa kwa lengo la kujadili maswala mbalimbali ambayo
yanaikumba secta hiyo barani africa na Tanzania kwa ujumla.
Amesema kuwa mkutano huo ambao ni wa 12 kufanyika kimataifa umelenga kutafuta fursa mbalimbali
za kutangaa biashara au bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na makampuni
mbalimbali nchini,kutoa elimu kwa wadau kuhusu maswala mbalimbali ya
usafirishaji pamoja pamoja na kutatua chanagamoto mbalimbali zinazokwamisha
secta hiyo hapa nchini na barani Africa.
“tunawaomba
wadau mbalimbali wajitokeze kwa wingi katika kuudhamini mkutano huu kwani ni
nafasi pekee ya makampuni ya kitanzania kutangaza bidhaa zao kupitia mkutano
huu kwa kuwa kutakuwa na watu kutoka maeneo mbalimbali Africa hivyo ni fursa
pekee”alisema masebo
Baadhi ya mada ambazo zinatarajiwa kuwasilishwa katika
mkutano huo ni pamoja na ajali za barabarani na jinsi ya kukabiliaa
nazo,usalama katika vyombo vya usafiri,kuibuka kwa dhana mpya katika logistic,msongamano
katika bandari,msongamano wa magari barabarani,pamoja na mada nyingi ambazo
zimetajwa kuwa ni manufaa kwa washiriki watakaoshiriki katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment