Mwanza, Jeshi la polisi mkoani Mwanza, linawashikilia watu 14 kwa
tuhuma za kuhusika na tukio la utekaji nyara wa mtoto mwenye ulemavu wa
ngozi Pendo Emanuel wa kijiji cha ndami wilayani kwimba tukio
lililotokea Desemba 27 mwaka jana.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya za
Misungwi, Kwimba na Sengerema Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa mulongo
amesema kuwa miongoni mwa watuhumiwa hao wamo waliohusika kwenye
utekaji wa mtoto huyo pamoja na wale waliomuhifadhi kwenye hoteli moja
jijini Mwanza kabla ya kumsafirisha kwenda kusikojulikana.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa Mwanza
Alfred Kapole pamoja na katibu wa chama hicho mkoani humo Enos Tuju
wameendelea kukemea ukatili dhidi watu wenye ulemavu wa ngozi Albino
pamoja na kuiomba serikali kudhibiti vitendo vya mauaji ya albino
yanayo endelea kutokea mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment