Katika hali isiyokuwa ya kawaida aliyekuwa
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa dare s salaam bwana JOHN GUNINITA leo
ametangaza kumpandisha mahakamani mkuu wa wilaya ya kinondoni DC PAUL MAKONDA kwa kila elichokiita kuwa ni
kudhalilishshwa na kutupiwa maneno ya kashfa.VIDEO IKIONYESHA SIKU MAKONDA ALIPOTOA MANENO HAYO
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dare s salaam
mh GUNINITA amesema kuwa kitendo alichokifanya DC MAKONDA cha kuitisha mkutano
wa wanahabari na kuwatukana viongozi wastaafu wa chama cha mapinduizi ni
kitendo ambacho hakivumiliki na mtu yoyote na kwa kuwa chama kimeshindwa
kumshughulikia sasa njia pekee anayoiona inafa kumwadhibu ni kwenda mahakani
ili haki ipatikane.
Amesema kuwa sio mara ya kwanza kwa kiongozi huyo aliyewahi
kuwa kiongozi wa umoja wa vijana CCM kulalamikiwa kwa kitendo chake cha utomvu
wa nidhamu mbele ya viongozi wenzake wa ndani ya chama hivyo sasa ni wakati
muafaka wa kuhakikisha kuwa wanamfundisha adabu kwa kutumia sheria za Tanzania.
Ameongeza kuwa chama cha mapinduzi kina utaratibu
wake wa kuwaonya wanachama wake pale wanapokwenda kinyume na utaratibu wa chama
hicho lakini kitendo cha kijana huyo kutoka nje mbele ya wanahabari kuwatukana
viongozi wa chama hicho ambao mbali na uongozi ni baba zake ni kitendo ambacho
sio utaratibu wa chama na hakina wa kuvumilia kitendo hicho
“sisi sio wa kwanza kutukanwa na MAKONDA,alianza
kututukana sisi na viongozi wengine,juzi amemtukana waziri mkuu mstaafu na
mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba tanzania jaji JOSEPH WARIOBA na
akaona haitoshi tumeshughudia akimpiga katika mkutano ambao yeye alienda kama
mwalikwa tu ni utomvu wa nidhamu wa hali ya juu na siamini kama chama
kjimemwacha kama alivyo”amesema GUNINITA.
Amesema kuwa MAKONDA ni kiongozi mdogo sana kwani
nafasi aliyokuwa nayo umoja wa vijana UVCCM yeye amekaa hapo kwa miaka kumi na
nafasi yake mpya ya ukuu wa wilaya yeye amekaa miaka 25 hivyo asitumie vyeo
vyake vya kuoteshwa kama uyoga kuwatukana wakubwa ndani ya chama hicho.
Paul makonda aliitsha mkutano wa wanahabari ambapo
aliwatuhumu mwenyekiti huyo mstaafu pamoja na viongozi wengine wastaafu wa
chama hicho akiwemo mzee msindai kuwa ni vibaraka wanaotumwa na baadhi ya
wasaka uraisi kukivuruguga chama cha mapinduzi.
KUHUSU CHAMA CHA MAPINDUZI
GUNINITA amesema kuwa chama cha mapinduzi kwa sasa
kimekuwa ni chama cha wakubwa na kupeana vyeo hivyo watu kama yeye hata
walalamike hadi mwisho hakuna wa kuwasikiliza tena na amejaribu kulalamika kwa
viongozi wa juu wa chama kuhusu MAKONDA lakini hakuna aliyemsikiliza na ndio
nmaana ameamua kwenda mahakamani kutafuta haki yake.
MWANASHERIA ALONGA
Naye mwanasheria ambaye anashgulika na kesi hiyo BENJAMEN
MWAKAGAMBA amesema kuwa mteja wao ameleta malalamiko ya kulalamika kuwa
amedhalilishwa kwa maneno hivyo wao kama wanasheria wameona kuwa ni kweli kuwa
mteja wao amedhalilishwa sana hivyo wameamua kwenda mahakamani kumshaki
MAKONDA.
Amesema kuwa baada ya kauli hizo za kongozi huyo wao
kama wanasheria walimwandikia bariua ya kumtaka aombe radhi mbele ya vyombo vya
habari pamoja na kulipa faini ya million mia moja lakini aliwajibu kuwa kauli
hizo hakuzitoa yeye bali ni maagizo kutokia kwa viongozi wa juu wa chama hicho
hivyo hawezi kuomba radhi kwa kauli hizo.
No comments:
Post a Comment