Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari
Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia
mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti
iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu
Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali
ambayo pia imewaudhi watu wengine.
Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali
ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe
sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya
Dar es Salaam bila kukosa.
Ni muhimu sana kwa Askofu Josephat Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala
ya Kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika
jamii.
Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili
unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.
No comments:
Post a Comment