WATU
15 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KULA NJAMA NA KUJARIBU KUMTOROSHA
ASKOFU GWAJIMA AKIWA HOSPITALINI.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia na kuwahoji watu 15
ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kula njama pamoja na kujaribu kumtorosha
Askofu Josephat Mathias Gwajima ambaye amelazwa katika Hospitali ya TMJ kwa
matibabu.
Mnamo tarehe 29/03/2015
majira ya saa tisa na dakika thelathini usiku watu hao 15 katika hali isiyo ya
kawaida walifika hospitalini hapo wakidai kwamba walikuwa wanataka kwenda
kumuona mgonjwa huyo. Askari ambao wapo katika lindo hilo waliwatilia mashaka
watu hao hivyo waliwakatalia kuingia. Kundi hilo la watu 15 lilijaribu kutumia
nguvu kuingia katika chumba alicholazwa askofu Gwajima lakini walikamatwa na kikosi
maalum cha Polisi ambacho kabla ya tukio hilo walikuwa wanafuatilia mwenendo wa
kundi hilo.
Baada ya kukamatwa
watuhumiwa hao walipekuliwa hapo hapo TMJ na kukutwa na Begi ambalo lilikuwa na
vitu mbalimbali kama ifuatavyo:
1.
Silaha ambayo ni Bastola aina ya BERRETA
yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu.
2. Risasi
17 za Shortgun.
3. Vitabu
viwili vya Hundi (Cheque Books)
4. Hati
ya kusafiria yenye jina la GWAJIMA JOSEPHAT MATHIAS yenye namba AB 544809.
5. Kitabu
cha Hundi cha EQUITY Bank.
6. Nyaraka
mbalimbali za kampuni ya PUMA
7. Chaja
ya Simu na Tablets
8. Suti
mbili na nguo za ndani.
Orodha ya watuhumiwa
waliokamatwa ni kama ifuatavyo:
1.
CHITAMA S/O MWAKIBAMBO, Miaka 32, Fundi
Selemala, Mkazi wa Gongolamboto.
2.
EDWIN S/O AUDEX, Miaka 24, Mchungaji,
Mkazi wa Kawe Maringo.
3.
ADAM S/O MWASELELE, Miaka 29, Mhandisi,
Mkazi wa Kawe Maringo.
4.
FREDERICK S/O FUSI, Miaka 25, Mkazi wa
Mbezi Beach.
5.
FRANK S/O JOHN MINJA, Miaka 24,
Mwanafunzi IMTU, Mkazi wa Mbezi Beach.
6.
EMMANUEL S/O NGWELA, Miaka 28, Mlinzi
Shirikishi, Mkazi wa Keko Juu.
7.
GEOFREY S/O WILLIAM, Miaka 30, Mhadhiri
UDSM, Mkazi wa Survey Chuo Kikuu.
8.
MATHEW S/O NYANGUSI, Miaka 62,
Mchungaji, Mkazi wa Mtoni Kijichi.
9.
BONIPHACE S/O NYAKYOMA, Miaka 30,
Mchungaji, Mkazi wa Kitunda.
10.
GEOFREY S/O ANDREW, Miaka 31, Dereva,
Mkazi wa Kimara Baruti.
11.
DAVID S/O MGONGOLO, Miaka 24, Mchungaji,
Mkazi wa Ubungo Makoka.
12.
GEORGE S/O MSAVA, Miaka 45,
Mfanyabiashara, Mkazi wa Ilala Boma.
13.
NICHOLAUS S/O PATRICK, Miaka 60,
Mchungaji, Mkazi wa Mbagala Mission.
14.
GEORGE S/O KIWIA, Miaka 37, Dalali wa
magari, Mkazi wa Tandale Uzuri.
15.
YEKONIA S/O BIHAGAZE, Miaka 39,
Mchungaji, Mkazi wa Kimara Stop Over.
Baada ya upekuzi
kukamilika watuhumiwa walifikishwa kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa mahojiano
zaidi ikiwa ni pamoja na kupata uhalali wa wao kumiliki silaha hizo na risasi
mpaka walipokamatwa.
Upelelezi wa shauri
hilo unaendelea kwa madhumuni ya kubaini sababu za njama hizo sambamba na kujua
mbinu zote zilizotumika kutaka kufanikisha jaribio la kumtorosha Askofu
Josephat Mathias Gwajima.
S.
H. KOVA
KAMISHNA
WA POLISI KANDA MAALUM
DAR
ES SALAAM
No comments:
Post a Comment