BANGI
ni dawa ya kulevya iliyopo kwenye kundi la dawa za kulevya lenye kuleta Njozi
(Hellucinogences).Vileta njozi huathiri ubongo na kumfanya mtumiaji kutoa
tafsiri potofu ya hisia na kujisikia kama vile yuko nje ya dunia.
Mtumiaji
wa bangi huzalishwa na kutumiwa kwa wingi barani Afrika kwa sababu hustawi
maeneo mengi.
Nchini
Tanzania kanda ya nyanda za juu kusini, mkoani Njombe wilayani Makete hustawi
zaidi.
Wakati
Serikali ikiamini kuwa gerezani ni mahala salama hata kuwatunza wanaokamatwa na
dawa za kulevya, hali si shwari katika baadhi ya magereza hapa nchini, kutokana
na ongezeko la matumizi ya dawa hizo.
Baadhi
ya askari Magereza, wafungwa na mahabusu katika magereza mbalimbali hapa
nchini, wanahusishwa na biashara ya dawa za kulevya ndani ya magereza,
imebainika.
Uchunguzi
uliofanywa kwa miezi miwili sasa, umebaini kuwepo kwa dawa za kulevya katika
magereza mengi hapa nchini, hususani Bangi.
Baadhi
ya askari ambao hawakutaka kutajwa majina yao na vyeo katika Gereza la Ruanda
na Songwe mkoani Mbeya, walithibitisha kuwepo kwa uingizwaji wa bidhaa hiyo
ambayo inafanyika kwa siri kubwa katika magereza hayo.
Biashara
hiyo inahusisha baadhi ya askari, wafungwa na mahabusu wenye kesi mbalimbali,
wanaokaa muda mrefu gerezani huku kesi zao zikiahirishwa mara kwa mara.
Baadhi
ya waliowahi kuwa mahabusu wa gereza la Ruanda mkoani Mbeya, wanaeleza kuwa
wahusika wakubwa ni baadhi ya wafungwa wanaofanya kazi nje ya gereza, kisha
kurejeshwa alasiri na baadhi wanaopelekwa mahakamani kusomewa mashitaka ya kesi
zinazowakabili.
Wanasema
njia ambazo zinatumika kuingiza dawa hizo gerezani ni kujiingiza katika sehemu
ya haja kubwa wakiwa nje ya gereza na wakati wa ukaguzi unapofanyika kwa kila
anayeingia gerezani hapo, askari wanashindwa kubaini.
“Baadhi
ya wafungwa ambao wanakaribia kumaliza muda wao, wanatolewa kwenda kufanya kazi
za nje ikiwemo kwenda kukata nyasi za Ng’ombe na kurejeshwa mchana na wale
wanaoenda kusaga mashine wanaweka kwenye unga. Hao wana mtandao na wauza bangi
uraiani, wanaingia nazo na kufanya biashara ndani ya gereza, mle kuna biashara
nyingi” anaeleza mmoja wa aliyekuwa mahabusu katika gereza hilo na kuachiliwa
huru hivi karibuni baada ya Mahakama kuona hana hatia.
Baadhi
ya askari mgambo wanaotumwa kuwachukua mahabusu na kuwapeleka katika mahakama
za mwanzo, ambao nao waliomba hifadhi ya majina yao, walikiri kuwepo kwa
biashara hiyo ambapo walisema kuwa, biashara hiyo inafanyika kutokana na vipato
vidogo vya Mgambo na askari Magereza kutokuwa na mianya ya rushwa tofauti na
askari polisi.
Mbali
na bangi, wanasema kuwa, katika magereza pia kuna uvutaji mkubwa wa sigala
ambazo huingizwa kwa njia za haja kubwa kisha kutolewa vyooni na kuhifadhiwa
katika maeneo mbalimbali ya sero na nje ya sero bustanini.
Wakala
wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali, idara ya huduma za sayansi ya makosa ya
jinai (GCRLA), inataja madhara yanayowakuta watu wanaotumia dawa hii ya kulevya
kuwa ni kuwaza, kuona, kusikia na kuhisi vitu kwa namna tofauti au
visivyokuwepo, kupata njozi, kuongezeka kwa hamu ya kula, kuwa kama kichaa,
kutapika, wasiwasi, hamaki na kupumbaa.
Madhara yatokanayo na matumizi ya muda mrefu
Madhara
hayo ni kupata ugonjwa wa akili, mabadiliko ya maono, hisia na mtizamo
yasiyoisha, kuharibika kwa ubongo na kusababisha kupungua kwa uwezo wa
kukumbuka na kufikiri na kukosa ari ya maendeleo na mabadiliko ya aina yoyote
ile.
Sheria inasemaje kuhusu bangi
Kutumia,
kuhamasisha matumizi, kuuza, kusafirisha, kuhifdhi au kujihusisha kwa namna
yeyote ile na bangi ni kosa la jinai. Adhabu kwa makosa haya hufikia hadi
kifungo cha maisha.
Sheria inasemaje kuhusu bangi
Kutumia,
kuhamasisha matumizi, kuuza, kusafirisha, kuhifdhi au kujihusisha kwa namna
yeyote ile na bangi ni kosa la jinai. Adhabu kwa makosa haya hufikia hadi
kifungo cha maisha.
Mbali
na tatizo la Bangi, moja ya matatizo yanayotajwa ni suala la kutumia kwa
kubadilishana vitu vyenye ncha kali zikiwemo nyembe.
“Nilikamatwa
na kupelekwa gerezani mwaka 2011, nikakuta watu wananyolea wembe mmoja ambapo
kilichoniuma
ni kwamba kuna rafiki yangu aitwaye Jack, alikuwa anaishi na
VVU, alinyolea wembe akajikata, akampa jamaa anaitwa Kamugisha akajikata, naye
akampa Side, naye akajikata na Side alimpa Chidi akatie kucha naye akajikata,
virusi vikasambaa kwa wote”anasema Frank Kaitaba, kijana ambaye alikuwa
mtumiaji wa dawa za kulevya Jijini Dar es Salaam na sasa anahudumiwa na shirika
la Medecin De Munde la Temekelinalopunguza athari za madawa ya kulevya..
Anasema
baada ya hapo akaamua kuwafuata madaktari wa gereza hilo na kuanzisha kikundi
cha uelimishaji rika ndani ya gereza na kwamba tangu hapo ndani ya gereza hilo
mtu anapotaka kunyoa anampa taarifa kiongozi aitwaye Onyango, ambaye anatoa
wembe na kumwamuru nyapala asimamie matumizi ya nyembe.
SOURCE JAMII FORUM
SOURCE JAMII FORUM
No comments:
Post a Comment