CAPTAIN KOMBA ALIKIONA KIFO CHAKE,TIZAMA KAULI YAKE YA MWISHO KWA WANAWE
Kifo cha Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa CCM kapteni John Komba ambaye amefariki dunia akiwa hospital ya TMJ February 28 kilitanguliwa na kitu ambacho kinadhaniwa kama kilikua ni ishara kwa familia yake.
Claudia John Komba ambaye ni mtoto wa 9 kati ya watoto 11 wa Mheshimiwa John Komba ameongea na wanahabari na kuelezea baadhi ya vitu ambavyo kwao imekua kama kauli ya mwisho kwa Baba yao ambayo aliitoa siku ya sherehe ya kuzaliwa kwake.
Claudia alianza kwa kusema>>’Taarifa ilinifikia mida ya saa 9 akasema anajisikia vibaya wakati yupo njian akawa anaweweseka sana,tulipofika TMJ hospital walipofanya vipimo walisema ameshafariki’
Mwandishi:Kabla ya hapo kulikua na ripoti ya mzee kuugua?
Claudia John Komba:Zilikuwepo baba alikua amekaa ilikua mida ya asubuhi akawa analalamika anajisikia vibaya vibaya tukampeleka hospital ya Sanitas iliyopo Baraka Plaza,tukagundua sukari imepanda sana na presha imepanda sana,akatolewa akawa anaendelea vizuri,juzi tarhe 26 feb ilikua siku yangu ya Birthday’
‘Akaita watoto wote akasema nataka kufanya birthday hii kwa sababu birthday nyingi huwa zinanioita nakua nipo nje kwa hiyo birthday hii nataka nifanye kwa hiyo akatukusanya watoto wote,aliongea maneno ya mwisho akatusihi watoto tupendane tusiweke matabaka kwamba huyu mdogo huyu mkubwa alisema yeye hana mkataba na Mungu’.
No comments:
Post a Comment