_____________
Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao
ya kijamii kuhusu hali ya Afya ya Naibu
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai. Ofisi ya Bunge inapenda kuutangazia umma na Wananchi wote kuwa,
taarifa hizo zinazosambazwa katika baadhi ya Mitandao si za kweli, bali ni uzushi mtupu.
Ukweli ni kwamba Naibu Spika wa Bunge, Mhe.
Job Ndugai ni Mzima wa afya na hivi sasa
yuko jimboni kwake Kongwa, Mkoani Dodoma akifanya maandalizi ya Mwisho ya Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg.
Abdulrahman Kinana itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii na hasa Jimboni Kongwa, Dodoma.
Ofisi ya Bunge inapenda kuwatoa hofu
Wananchi wote na kuwataka kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa si za kweli bali ni
uvumi unaonezwa na watu wachache wenye nia ovu ya kujenga hofu miongozni mwa Wananchi kupitia
mitandao ya kijamii.
Aidha
tunapenda kutoa rai kwa watu wote kuacha kusambaza taarifa hizo potofu na badala yake kama kuna taarifa zozote kuhusu
Ofisi ya Bunge au Viongozi wake wafanye jitihada za kuthibitisha taarifa hizo
kwenye Mamlaka husika kabla za kuzisambaza. Ofisi ya Bunge inao utaratibu rasmi
wa kutoa taarifa muhimu kwa wananchi na umma kwa ujumla, hivyo si vyema kwa
watu kusambaza taarifa potofu kuhusu Bunge na viongozi wake ambazo zinaweza kuleta usumbufu
miongoni mwa Viongozi na baadhi ya wananchi.
Imetolewa na: Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
4 MACHI 2015
No comments:
Post a Comment