Friday, March 6, 2015

VPL KUENDELEA WIKIENDI HII

Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki kwa viwanja sita kutimua vumbi, michezo mitatu ikifanyika siku ya jumamosi na michezo mingine mitatu kufanyika siku ya jumapili.

Katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro watawakaribisha maafande wa Ruvu Shooting kutoka Mlandizi, Coastal Union watakua wenyeji wa Kagera Sugar kwenye dimba la Mkwakwani,  huku JKT Ruvu wakiwakaribisha Azam FC katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Jumapili Mgambo JKT watakua wenyeji wa timu ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Mtibwa Sugar wakiwa wenyeji wa wagonga nyundo timu ya Mbeya City katika Uwanja wa Manungu Turiani.

Katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam watani wa jadi Simba SC watakuwa wenyeji wa Young Africans, mchezo unaotarajiwa kuanzakutimua vumbi majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

No comments: