Thursday, April 30, 2015

BODI YA AFYA WILAYA YA HAI YATOA RIPOTI YAKE OKTOBA 2010 HADI 2014 HAI

IMEELEZWA kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizopo katika hosipitali ya Wilaya ya Hai Bodi ya Afya wilayani hapo imeweza kufanya kazi ya kuziondoa changamoto hizo ili wananchi waweze kupokea humuda ya afya kwa njia stahiki.

 Hayo yameelezwa hii leo na Mganga Mkuu Wa Hosipitali ya Wilaya Paul Chaote katika mkutano wa Bodi ya Afya ulio ambatana na uteuzi wa Mwenyekiti Mpya wa kuongoza Bodi hiyo kutokana na Mwenyekiti aliye kuwa madarakani kumaliza muda wake kutokana na utaratibu uliowekwa kumalizika.

 Amesema kuwa Bodi ya afya ya Wilaya inayomaliza kipindi chake ilisimikwa na kuanza kazi rasmi mwezi oktoba mwaka 2010 lengo ikiwa ni kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu lakini kutokana na kuchelewa mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wapya,Bodi hii iliendelea kuwapo madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi.

Aliongeza kuwa Katika kipindi cha miaka minne bodi kwa kushirikiana na timu ya uendeshaji shughuli za afya pamoja na Menejimenti ya Halmashauri ilifanya mambo mbalimbali ikiwamo Kuongeza wigo wa huduma katika hosipitali ya wilaya kwa kufanya upanuzi kutoka majengo 7 mwaka 2010 hadi majengo 11 mwaka 2014.

Chaote aliongeza kuwa mambo mengine ni pamoja na Kufanya ukarabati katika vituo vya Afya na Zahanati,Kuongeza vituo vya hiduma toka 60hadi 62,Kufanya ziara elekezi za usimamizi katika hosipitali ya Wilaya nay a Machame,Vituo vya Afya na Zahanati na Kuingia mikataba 3 ya kiushirikiano kuendesha vituo vya makanisa ikiwa ni pamoja na hosipitali teule ya Machame.

 Pia tumeweza ku Kufanya uhamasishaji wa mfuko wa afya ya jamii katika mikutano ya wananchi,mikusanyiko ya watu kama masokoni,makanisani na misikitini,katika shule za sekondari na kuongeza wanachama kutoka kaya 854 mwaka 2010 hadi kaya 5,028 mwaka 2014,Kufungua akaunti katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali.

 "Ni jambo la kunivunia kuona kuwa licha ya changamoto nyingi zinazo jitokeza ndani ya hosipitali yetu na vituo vingine fya Afya bado Bodi ya Afya imeweza kutoa huduma kwa wananchi pamoja na kuwaelimisha kuhusu bima za afya ili kila kaya iweze kupokea matibabu yaliyo bora kpitia bima ya Afya."Alisema Chaote.

Alisema kuwa mbali na mafanikio hayo yote pia wameweza kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo uchangiaji mdogo wa wananchi katika masuala ya mfuko wa afya ya Jamii ambapo lengo la kitaifa ifikapo disemba 2015 ni 30% wakati wilayaya Hai bado ni 10%tu,uchakavu wa majengo katika baadhi ya vituo,ukosefu wa huduma za maabara katika zahanati za Serikali ukosefu wa baadhi ya huduma muhimu katika Hosipitali ya Wilaya kama nishati mbadala wakati umeme wa Tanesco unapo katika.

 "Tunaamini kwamba Bodi hii iliyo undwa itasimamia kamati zote zilizoko chini yake na itahakikisha kuwa huduma za Afya katika Wilaya yetu zitaboreshwa katika viwango vinavyopendekezwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Nina kuomba sasa uzindue rasmi Bodi hii ambayo itafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu."alisema Chaote.

 HABARI KATIKA PICHA WAKATI WA UPIGAJI KURA WA KUCHAGUA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA BODI MPYA YA MAJI HAI.

Mganga Mkuu wa Hosipitali ya Wilaya ya hai Paul Chaote aliye simama akizungumza jambo wakati wa kikao cha kuchagua wajumbe wa Bodi ya Afya Wilaya.

Wajumbe wa Bodi ya Afya Wilaya wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Hosipitali ya Wilaya Hai

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Afya Wilaya  katikati Bw Inocavity Swai akisikiliza maelezo mara baada ya upigaji kura kumalizika.

Dr Saitore Laizer akitoa neno la shukrani kwa wajumbe mara baada ya zoezi la kura kumalizika.

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Afya aliye vaa  shati la Blue akipongezwa na Mwenyekiti aliye maliza muda wake.

Mwenyekiti aliye maliza muda wake Joel Niwakoeli Nkya akitoa neno la shukrani kwa Wajumbe wa bodi ya Afya Wilaya mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi.



Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Aya akisisitiza jambo wakati akiahidi mambo atakayo yafanya wakati wa muda wake.

No comments: