MKUU wa wilaya ya Hai Antony Mtaka amempongeza aliyekuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Askofu Mstaafu Erasto N kweka kwa jitihada zake alizozifanya wakati akihudumu kama askofu ikiwamo kupokea miradi mbli mbali ya maji iliyopitia katika Dayosisi Hiyo.
Mtaka ameyasema hayo hii leo wakati wa kikao cha kumchagua mwenyekiti na wajumbe wa bodi ya maji ya Lyamungo Umbwe kilichofanyika katika shule ya sekondari Lyamungo.
Amesema kuwa ni mfano wa kuigwa kwa kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele katika kuiletea jamii maendeleo pasipokuwa na ukiritimba, ubadhirifu na kuweka maslai binafsi ya shughuli za kimaendeleo.
“ ni jambo la bahati sana kwa Askofu Kweka kutanguliza maslai ya Wananchi katika mradi huu wa maji pasipo kujali atanufaika vipi, ingekuwa ni mtu asiyekuwa mwadilifu angegeuza mradi kuwa wake huku wananchi wakiangamia kwa ukosefu wa maji safi na salama.” Alisema Mtaka
“Askofu Kweka alipoke Euro mill. 34 sawa na shilingi Bill. 68 mwaka 1992 ambapo ndipo mradi huo ulianza rasmi ukijumuisha vijiji 11 kutoka Hai na Vijiji 13 kutoka Moshi vijijini, ingekuwa ni mwingine angepeleka wapi?” Alihoji Mtaka
Sanjari na hayo amewataka viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza bodi hiyo ya Lyamungo Umbwe kuepuka kuchanganya siasa na kazi za miradi ya maendeleo ili miradi hiyo iweze kuwanufaisha wananchi wote na vizazi vya baadae.
“epukeni kutapeliwa na wanasiasa wanaojiingiza katika miradi ya kimaendeleo kwani wengi wao ni wapotoshaji kwa kuingiza siasa katika utendaji” alisema Mtaka.
Kwa upande wake mhandisi wa maji wilaya ya Hai ambaye pia alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo Mhandisi Nyakaraita Mwita amewataka wajumbe waliochaguliwa katika bodi hiyo kupeanan ushirikianano katika utendaji ikiwemo pamoja na kushirikiana na halmashauri ili kuleta ufanisi zaidi.
Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kuopata maji safi na salama kama bodi ya maji ilivyojusudia ili kuepuka mnagonjwa mbali mbali yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.
Pia amesema kuwa wanawake wamekuwa ni waathirika wakubwa wa utafutaji wa maji safi na salama katika familia zao jambo linalowapelekea kushindwa kushiriki katika shughuli nyingine za kimaendeleo.
Katika zoezi la upigaji wa kura wajumbe walikuwa 258 ambapo kura moja iliharibika huku Michael Sitaki Mmasy akishikilia nafasi ya mwenyekiti,Emmanuel Izack Show akiwa ni makamu mwenyekiti ambapo walipita bila kupingwa kutokana na kutojitokeza kwa wagombea wengine kuchukua fomu za nafasi hizo kama ilivyotakiwa.
Kwa upande wa wajumbe watendaji wa bodi ya maji, Bibianna Mmasy aliibuka mshindi kwa kupata kura 85 na Bi, Joyce Kweka akipata kura 71 ambazo zote kwa pamoja zilivuka asilimia hamsini iliyoitajika.
|
No comments:
Post a Comment