Thursday, April 30, 2015

KIMEELEWEKA--UKAWA WATOKA CHIMBO MUDA HUU,SOMA WALICHOAMUA SASA

Viongozi wakuu wa vyama vikuu vya upinzani UKAWA wakiwasili makao makuu ya CUF kwa ajili ya kuzungumza na wanahabari leo
Hatimaye viongozi wa vyama vikuu vya upinzani vinavyounda  UKAWA wameibuka upya na kutangaza rasmi kutokuwa na kutokuwa na imani na tume ya taifa ya uchaguzi nchini kwa kudai kuwa serikali ya chama cha mapinduzi inaitumia tume hiyo kutaka kusogeza uchaguzi mbele kwa lengo la kujiongezea muda wa kutawala.


Akisoma maadhimio ya umoja huo baada ya kukutana ndani ya siku mbli jijini Dar es salaam mwenyekiti mwenza wa umoja huo ambaye ni mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi mh JAMES MBATIA amesema kuwa kutokana na hali ya hewa inayoendelea kuhusu sintofahamu ya daftari la kupiga kura ni wazi kuwa sasa umoja wao hauna inami hata kidogo na tume ya uchaguzi kwani imeonyesha wazi kuwa inashirikiana na serikali ya chama cha mapinduzi kutaka kuhujumu uchaguzi ujao na kisha kuongeza muda wa uongozi wa serikali hiyo kwa kisingizio cha kutokumalizika kwa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Amesema kuwa tume ya taifa ya uchaguzi hadi sasa ikiwa imesalia takribani miezi mitatu pekee kuanza kwa kampeni rasmi za uchaguzi haijaanza wala hakuna dalili za maandalizi yoyote ya kufanyika kwa uchaguzi huo jambo ambalo linazidi kuleta wasiwasi kwa watanzania na kuamini kuwa kuna njama za kuahirisha uchaguzi huo kama ilivyofanyika kwa daftari la kudumu la wapiga kura.


“kuna jambo linashangaza sana,hadi sasa hakuna maandalizi yoyote yanayoashiria kuwepo kwa uchaguzi huo ilihali imebaki miezi sita tu kufanyika kwa uchaguzi huo,hakuna utaratibu wa vifaa vya uchaguzi huo,ambapo miaka iliyopita imekuwa ikifanyika maadalizi mwaka mmoja kabla lakini uchaguzi huu hadi leo hakuna maandalizi ya kuonyesha kuwa uchaguzi huo upo japo kuwa mwenyekiti wa tume hiyo anazidi kuwdanganya watanzania kuwa uchaguzi huo upo”.aliseama mh MBATIA.
Naye mwenyekiti wa CHADEMA mh FREMAN MBOWE amesema kuwa hakuna njia yoyote ya kuzia mabadiliko ambayo yanataka kufanywa na ukawa kwa sasa hivyo tume hiyo isikubali kutumika na serikali na badala yake ni lazima uchaguzi ufanyike mwaka huu kwa njiia yoyote.


MGOGORO KUHUSU MAJIMBO


Wakati huo huo UKAWA  umetangaza rasmi mchakato wao wa kugawana majimbo ambapo mwenyeikiti mwenza wa umoja huo mh MBATIA amesema kuwa hadi sasa mchakato huo unaendelea viruzi ambapo  majimbo 227 sawa na asilimia 95 ya majimbo yote Tanzania yameshapata wagombea huku majimbo 12 yakiwa yamesalia huku akisema kuwa ni maridhiano ndio yanaendelea na hakuna mgogoro kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Akizngumzia habari ambazo jana zilienezwa na baadhi ya magazeti nchini zikimtaja mwenyekiti wa NCCR mageuzi mh JAMES MBATIA kuandika barua ya kujiondoa katika umoja huo kwa kile kilichotajwa kuwa ni kutoridhika na mchakato wa ugawanaji wa majimbo hayo,MBATIA amesema kuwa UKAWA walisikitishwa sana na taarifa hizo za upotoshaji jambo ambalo amesema kuwa ni uzushi ambapo amesema kuwa taarifa hizo zina lengo la kuhujumu umoja huo na kuipa nafasi CCM jambo ambalo halitakubalika katika kipindi hiki ambacho watanzania wanahitaji mabadiliko.

Akizungumzaia taarifa hizo mwenyekiti wa chadema mh MBOWE amesema kuwa huu ni wakati ambao mambo mengi sana yataibuka ya kuzusha ili kuwagombanisha lakini wapo tayari kupambana na taarifa hizo na hakuna wa kuwagombanisha.
“Hakuna wa kuwatenganisha UKAWA kwa sasa,najua tunawindwa sana na watu ili tugombane ili watu wapate cha kusema,nasema hivi hakuna kitu kama hicho na hakivunjiki kitu hapa tupo imara na tupo GADO kupambana hadi dakika ya mwisho”,amesema Mh MBOWE.
Akizungumzia mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia umoja huo mwenyekiti wa chama cha NLD mh DK EMANUEL MAKAID amesema kuwa watanzania watulie kwani mgombea tayari ameshapatikana na muda wa kumtaja ukifika watamtaja lakini sasa ibaki kuwa siri kwani kuna baadhi ya vyama bado hata havina mtu wa kumsimamisha katika nafasi hiyo ya urais.

No comments: