RAIA
WATATU WA KIGENI WAKAMATWA KWA MAKOSA YA WIZI WA MTANDAO KATIKA MABENKI JIJINI
DAR ES SALAAM.
Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa watatu raia wa kigeni kwa makosa
yanayohusiana na wizi wa mtandao kwa lengo la kuiba katika vyombo vya fedha kama mabenki, maduka
ya kubadilishia fedha (Bureau de Change) au kuingilia miamala ya fedha
zinazosafirishwa na wateja kutoka nje na ndani ya nchi.
Polisi wa kikosi Maalum
cha kupambana na wizi wa mtandao (Cyber Crime) walipata taarifa za kuaminika
kwamba watu hao watatu walikuwa katika mazingira ya kutiliwa mashaka na ndipo
Polisi walienda Mtaa wa Mindu eneo la Upanga na kuwakamata. Watu hao walikutwa
katika nyumba namba 416 iliyopo katika ghorofa ya nne na walitambuliwa kwa
majina yafuatayo:
1. FOTIOS
S/O VOGIATZIS, Miaka 32, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Raia wa nchini
UGIRIKI mwenye Passport namba AK2669977.
2. ATHANASIOS
S/O VOGIATZIS, Miaka 30, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Mkazi wa Ugiriki
mwenye Passport namba AK3049876.
3. PANAGIOTIS
S/O ANGELIDIS, Miaka 25, Mkazi
wa Upanga, Raia wa UGIRIKI mwenye Passport namba AK2644930.
Watu hao watatu ambao
ni raia wa nchini Ugiriki kumbukumbu zao zinaonyesha kwamba wamekuwa wakiingia
na kutoka nchini Tanzania na kwenda nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya katika
namna ambayo inaonyesha kuwa ni wahalifu wa kimataifa kupitia mitandao.
Katika upekuzi watu hao
wamekamatwa na vielelezo mbalimbali vinavyopashiria njama zao kama ifuatavyo:
1.
Muhuri mmoja wa kughushi ulioandikwa
“Inspector General of Police DSM”
2. Nyaraka mbalimbali za kughushi za Polisi
Tanzania zinazowasaidia kwa lengo la
kupata malipo ya bima nje ya nchi ambazo zina mihuri ya kughushi.
3.
Zimepatikana Kompyuta Mpakato (Laptops)
zipatazo tisa ambazo watuhumiwa hawa huzitumia kwa ajili ya mawasilisano pamoja
na uhalifu huo wa kimataifa.
4.
Zimekamatwa laini za simu za mkononi (Cheap)
za kampuni ya simu ya Airtel ambazo baadhi zimetumika na nyingine hazijatumika.
5.
Aidha, zimekamatwa kadi mbalimbali za
benki (Credit Cards) zipatazo 13 zinazotumika kutoa fedha, kuingiza fedha, au
manunuzi mengine za ATM.
Pia watuhumiwa hao
wamekamatwa na vitabu vitano vyenye kumbukumbu za majina, anwani, pamoja na
namba za siri za wateja mbalimbali wa mabenki mbalimbali kutoka nchi za
Tanzania, Zambia, Afrika Kusini, Kenya, Uingereza na Nigeria.
Uchunguzi ziadi
unaendelea kuhusu raia hao watatu kutoka nchi ya Ugiriki ili kubaini mtandao
wao na kugundua matukio mbalimbali ambayo wameyafanya.
TAHADHARI
KWA WANANCHI NA WAGENI WENGINE
Pamoja na kuibuka na
wimbi hili la wezi wa mtandao bado ni salama kuweka na kutoa fedha katika
mabenki hapa nchini. Hata hivyo kutokana na wimbi hili la wizi kwa njia ya
mtandao, ni muhimu sasa kuzuia uhalifu wa aina hii kwa ushirikiano kati ya
wamiliki wa mabenki na wateja wao. Jeshi la Polisi linashauri (pamoja na
maelekezo mengine ya benki) njia sahihi ya kwanza ya kuzuia ni kuhakikisha
kwamba miamala yote inayofanyika katika akaunti za benki ni lazima ifahamike
kwa mteja kwa njia zifuatazo:
1. Mteja
ajulishwe kwa simu ya mdomo ili kuthibitisha muamala.
2. Mteja
atumiwe ujumbe kwa kila muamala unaofanyika kupitia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS)
kumjulisha mteja kiasi kilichotolewa, kiasi kilichoingizwa au makato au
maingizo yoyote kwa muda ule ule.
Aidha tunawaomba
wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi na wasikubali kutoa nambari
za akaunti zao kwa watu wasiohusika au nambari zao za siri hata kwa mtu ambaye
ni ndugu wa karibu sana.
Mara baada ya upelelezi
kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment