MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea msaada wa jezi seti 100 na mipira 50 kutoka kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), ambavyo vina thamani ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya mashindano ya mpira wa netibali na mpira wa miguu yatakayoitwa Kinondano Cup. Akizungumzia msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kinondani, Paul Makonda alisema mikakati yake ni kuhakikisha kuwa vijana wa Wilaya hiyo wanatumia vipaji vyao kujikwamua katika umaskini.
Makonda alisema mashindano hayo yatakuwa ni mpira wa miguu wanaume na wanawake, mpira wa kikapu wanawake na wanaume na mpira wa netibali ambao ni wanawake pekee."Nimedhamiria kuhakikisha kuwa jamii inaondokana na dhana kuwa wakazi wa wilaya hiyo ni watumia madawa na uchangudoa na njia sahihi ni kuwahusisha vijana na kutumia vipaji vyao," alisema.
Akizungumza baada ya kutoa msaada huyo Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy ambacho ndio wametoa mtaasa huo kupitia TSN, Khamis Tembo alisema msaada huo una lengo la kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Tembo alisema kampuni ya TSN inatambua umuhimu wa michezo hivyo kupitia Chilly Willy wameona ni muhimu kutoa msaada huo wa jezi seti 100 na mipira 50 ili kufanikisha malengo hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Smart Sport, George Wakuganda ambaye kampuni yake imetoa mipira 50 alisema wameamua kuungana na Mkuu wa Wilaya kwani wao ni wanamichezo.Wakuganda alitoa wito kwa wadau wengine kuungana na Mkuu huyo wa Wilaya kwani jitihada zake za kuhakikisha vijana wanatoka katika dibwi la umaskini ni za maana.(Imeandaliwa na mtandao wa http://www. habarizajamii.com/"
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda, akizungumza katika mkutano huo baada ya kutoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda (kushoto), akimkabidhi DC Makonda mpira mmoja kati ya 50 aliyoitoa kwa ajili ya mashindani hayo. |
No comments:
Post a Comment