Chama cha wananchi CUF
kimesema kuwa ni ukweli usipingika kuwa kwa sasa serikali ipo Taabani kutokana
na mambo mengi yanayotokea huku serikali ikiwa haitoi majibu yanayowaridhisha
wananchi jambo ambalo limewafanya watanzania kukata Tamaa na nchi yao.
Akifungua kikao cha kawaida
cha baraza la uongozi Taifa la chama hicho mwenyekiti wa CUF mh IBRAHIM HAROUNA
LIPUMBA amesema kuwa swala la sintofahamu juu ya mchakato wa uandikishwaji wa
daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na mchakato mzima wa upigaji kura
imeonyesha wazi kuwa serikali ya tanzania imeshindwa kufanikisha zoezi hilo
huku ikiitupia mzigo wote tume ya taifa ya uchaguzi ambayo na yenyewe
imeshindwa.
Amesema kuwa kushindwa
kumalizika kwa uandikishwaji wa Daftari hilo kwa muda uliopangwa ni jambo
ambalo lilikuwa haliepukiki kwani vyama vya upinzani pamoja na wadau mbalimbali
walishaitahadharisha serikali juu ya mchakato huo lakini serikali ilishindwa
kusikiliza kilio chao na matokeo yake mchakato huo umeshindwa kuafanikiwa.
Amesema kuwa moja ya
ajenda za kikao hicho cha baraza kuu la uongozi la chama hicho ni pamoja na
kujadili maswala hayo uyanayohusiana na kushindwa kufanikiwa kwa daftari hilo
la wapiga kura na kujadili nini cha kufanya ili uchagauzi uweze kufanyika na
pia ufanyike kwa amani na upendo.
Aidha Pr LIPUMBA
amesema kuwa serikali ya tanzania imeshindwa kuwa sikivu kwa wananchi wake
ambao ndio waliowaweka madarakani huku akitolea mfano sakata la migomo ya
wafanyabiashara,madereva na mambo mengine yanayoendelea ambapo amesema badala ya
serikali kukaa chini na watu hao ili kuwasikiliza imekuwa kinyume kwani
wamekuwa wakitumia ubabe na kuwaacha walalamikaji hao kukosa la kufanya.
Picha tatu juu ni baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho kilichoanza leo jijini Dar es salaam |
Katika hatua nyingine
mwenyekiti huyo amesema kuwa kikao hicho cha kawaida cha baraza kuu la uongozi
la taifa ambacho kitaketi kwa siku mbili mfululizo pamoja na mambo mengine watajadili muungano wa
chama chao pamoja na vyama vingine vya upinzani umoja uliopewa jina la UKAWA
pamoja na kujadili ni jinsi gani ya kuimarisha umoja huo kuelekea uchaguzi ujao
mwishini mwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment