Jana Kaimu Katibu Mkuu
John Mnyika amezindua mafunzo hayo kwa Kanda ya Victoria (Mwanza, Kagera na
Geita), ambapo amezungumzia masuala 2.
Suala la ajali ambalo
linaendelea kumwaga damu na kukatisha damu za Watanzania wenzetu kila kukicha
bila kuwepo kwa mkakati wowote wa kushughulikia wala uwajibikaji.
Baada ya kikao hicho
cha mafunzo kusimama kwa dakika moja kuwakumbuka marehemu waliokufa jana kwenye
matukio mawili tofauti, akitoa hotuba ya ufunguzi, Mnyika amemtaka Rais Kikwete
kutoendelea kutoa pole kwa wafiwa bila kutoa kauli ya mkakati wowote ambao
serikali inao katika kushughulikia suala la ajali ambalo alisema linapaswa
kutangazwa kuwa ni janga la taifa.
Ameendelea kumtaka
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta kuweka hadharani ripoti ya Kamati iliyoundwa
na mtangulizi wake, Harrison Mwakyembe, mwaka jana kuchunguza vyanzo vya
kukithiri kwa matukio ya ajali zinazosababisha kupotea kwa maisha ya watu
wengi, wengine kuwa walemavu, wajane, yatima n.k huku pia nguvu kazi ya taifa
ikipotea.
Amehoji ukimwa wa Rais
Kikwete na Sitta wakati watu wanaendelea kupoteza maisha huku hadi sasa kukiw
ahakuna uwajibikaji wowote ule kutokana na janga hilo.
Amezungumzia suala la
BVR na hatima ya uchaguzi mkuu.
Amesema kuwa majibu ya
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lubuva kwa kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA kuhusu
mchakato wa uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa BVR na suala la kusogeza muda
wa uchaguzi na hivyo kuongeza muda wa serikali iliyoko madarakani, hayajakidhi
haja, vigezo wala kuondoa shaka iliyopo sasa inayoibua kizungumkuti kikubwa kwa
taifa kuhusu hatma ya uchaguzi.
Amemtaka Jaji Lubuva
ili kumaliza shaka na kizungumkuti hicho cha kusogezwa kwa uchaguzi, NEC itoe
ratiba kamili yote ya uandikishaji wa wapiga kura kwa BVR, itakayoonesha tarehe
za zoezi zima litakavyofanyika, kata moja hadi nyingine, nchi nzima.
Ameitaka NEC kusema
tarehe ambayo vifaa vyote 8,000 vya uandikishaji (BVR kits) vitakuwa vimewasili
nchini kwa ajili ya kumaliza mchakato wa uandikishaji ndani ya muda ambao Jaji
Lubuva amesema zoezi litakuwa limekamilika.
Kwa sababu kwa
kuzingatia uozefu unaoendelea Mkoa wa Njombe, huku NEC ikitarajiwa kuandikisha
wapiga kura mil. 23.9 (kwa mujibu wa tume) nchi nzima, au mil. 24 (kwa mujibu
wa NBS), kiuhalisia mahesabu ya kawaida yanadhihirisha kabisa kuwa zoezi la
uandikishaji halitaweza kukamilika ifikapo mwezi Julai kama ambavyo Jaji Lubuva
amekaririwa akisema.
BVR
NA BOMU LA UFISADI; kwa kuwa baada ya mwongozo ulioombwa na
Mnyika bungeni kuhusu hatma ya BVR, kura ya maoni na hatma ya uchaguzi mkuu
mwaka huu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kuwa tayari serikali imeshatoa 75%
ya malipo ya BVR, lakini hadi sasa NEC haijaweza kufanya kutimiza wajibu wake
sawasawa ikiwemo kupatikana kwa vifaa (kulingana na malipo ya 75% aliyosema
PM), basi kuna haja ya Bunge kupitia Kamati ya Hesabu za Serikali kuingilia
kati na kukagua matumizi ya fedha hizo za walipa kodi wa Tanzania.
Amesema hivyo kwa
sababu katika masuala ya zabuni na mikataba lazima kila upande uwajibike
kulingana na utekelezaji wa mkataba wa shughuli husika.
Hivyo amesema mbali na
Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ambayo inapaswa kukutana na NEC kama
ilivyoagizwa bungeni, lakini pia PAC inapaswa sasa kuingilia kati kuangalia
mahesabu na matumizi ya fedha hizo kwenye mchakato wa BVR, maana kuna harufu ya
uvundo wa ufisadi.
KAMA UNAVYOONA KWENYE PICHA NI .Baada ya uzinduzi wa mafunzo ya kuwaandaa
viongozi wa chama kushinda dola na kuongoza serikali, hapa ni mkutano wa
hadhara Viwanja vya Furahisha, uliohutubiw ana Kaimu Katibu Mkuu, JJ Mnyika.
Kama ilivyo ada ya watu wa Mwanza, ambao walishaamua kwa maneno na vitendo
kuambatana na CHADEMA sasa pamoja na UKAWA kwa ajili ya mapambano ya kweli ya
kufanya mabadiliko ya kweli ya utawala na mfumo, mkutano wa leo ulikuwa mkubwa
huku wananchi wakifurahia kusikia masuala yanayohusu ustawi wao na taifa lao
yakijadiliwa.
Masuala kama vile janga la ajali linaloendelea kuchukua maisha ya Watanzania
wenzetu huku serikali ya CCM chini ya Rais Kikwete ikitoa rambirambi bila
kuweka mkakati wowote wa kunusuru maisha ya watu, masuala ya uandikishaji wa
wapiga kura na hatma ya uchaguzi mkuu yalipewa kipaumbele katika hotuba ya
Kaimu Katibu Mkuu Mnyika.
No comments:
Post a Comment