Thursday, April 2, 2015

NEWZZ--HAKUNA KURA YA MAONI TANZANIA


Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)imetanga rasmi kuhairisha kura maoni juu ya  Katiba inayopendekezwa ambayo ilitarajiwa kufanyika tarehe 30 Aprili mwaka huu mpaka pale watakapotangaza tarehe maalum baada ya kujiridhisha kuwa mchakato wa uandikishwaji wa daftari la kudumu bado haujakamilika.

 NA KAROLI VICENT
  Akitangaza kuhairisha zoezi hilo leo  jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Jaji Mstaafu Damiani Lubuva wakati wa Mkutano na vyombo vya Habari ambapo amesema  tume hiyo imefikia maamuzi ya kuhairisha kura ya maoni kutokana na sababu zilizojitokeza kwenye uandikishaji Mkoani njombe.
       
    Jaji Lubuva ameongeza kuwa kutangazwa kwa tarehe husika kutategemea maushauriano na tume ya uchaguzi wa taifa ya Zanzibar (ZEC).
     

        Aidha,Jaji huyo amesema kuwa kutokana na uhaba wa vifaa vya kuwaandikisha wananchi kuwa vichache tume hiyo imeshalipia vifaa vingine ambapo kwa mujibu wa jaji huyo amesema Shehena ya Vifaa vinatajiwa kuwasili kwa awamu tatu kwaanzia sasa.
     
    Amesema kuwa kwa hali iliyoshughudiwa mkoani njombe ambappo kulikuwa  na mashine 250 kwa sasa tume imeagiza vifaa vingi ili kuweze kuwaandisha wananchi kwa haraka zaidi ambapo amesema kuwa  vifaa vitakuja kwa awamu tano ambayo kwa sasa zinakuja mashine 268 baadae zitakuja mashine 1600 na ya mwisho 1600
      
 Jaji lubuva amebainisha kuwa vifaa hivyo vikija vyote zoezi zima la kuwaandisha wapiga kura litakamilika nchi nzima mwezi wa Julai.
       
        Vilevile Jaji lubuva amesema kwa sasa serikali imeshalipa gharaza zote za mashine ambazo anasema zimagharimu Dolla milioni 72.  

    Kuhusu kuaomba mashine za BVR nje ya nchi. Jaji lubuva amesema ni kweli tume hiyo ilikwenda nchi hizo na kuomba mashine hizo na kudai hilo ni jambo la kawaida kwani ni nchi rafiki.

Kuibuka huko kwa tume ya uchaguzi NEC inakuja ikiwa tayari wanasiasa mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Demokrasia maendeleo Chadema Freeman Mbowe kupinga zoezi hilo kwa mfumo wa BVR kusema ni vigumu kufanyika kwa wakati.
Kutokana na Tume hiyo kushindwa kumaliza kuwaandisha kwa wakati wananchi kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo mpya wa Biometric Voters Regislation,(BVR). nchi nzima kwa mwezi mmoja uliobaki.
        


No comments: