Thursday, April 2, 2015

COASTAL YAIPIGIA HESABU PRISON, YAWEKA MIPANGO YA KUHAKIKISHA POINTI TATU ZINABAKI MKWAKWANI


Timu ya Coastal Union ameanza kuzipigia hesabu pointi tatu muhimu zawapinzani wao Tanzania Prison ili kuweza kuhakikisha wanazichukua
wakati watakapokutana kwenye mechi ya Ligi kuu Tanzania bara.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM
Mkwakwani ikiwa ni mzunguko wa pili wa ligi hiyo ikielekea lala
salama.

Akizungumza leo mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo
yanayo endelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini
hapa,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kikubwa zaidi
wanachojivunia ni kuendelea kuimarika kikosi hicho.
 Kocha Mkuu wa Coastal Union ya Tanga,Jamhuri
Kihwelu "Julio"amimnyajua chini mlinda mlango wa timu hiyo,Shabani
Kado jana mara baada ya kumalizika mazoezi ya timu hiyo.



Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuiwezesha timu hiyo kupata
matokeo mazuri katika mechi zote zilizosalia ikiwemo kuwataka
wachezaji kutimiza wajibu wao wa kuipa ushindi timu hiyo.

Amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kupambana kufa na kupona ili
kumaliza ligi hiyo wakiwa nafasi tatu za juu kwenye michuano hiyo
ambayo msimu huu imeonekana kuwa na upinzani mkubwa.

Hata hivyo amewataka mashabiki pamoja na wapenzi kujitokeza kwa wingi
katika michezo yao iliyosalia ikiwemo ya ugenini na nyumbani ili kuipa
hamasa timu hiyo kufikisha malengo yao.



No comments: