Tigo
Tanzania jana imetoa vitu vya aina mbalimbali katika shule maalumu ijulikanayo
kama Sinza maalumu iliyopo jijini Dar es salaam katika kusherehekea mapumziko
ya sikukuu ya pasaka. Kampuni ya Tigo pia imelipia gharama ya matumizi ya umeme
ya hapo shuleni kwa mwaka mmoja.
Akizungumza
katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika shuleni hapo, Meneja mkuu wa Tigo
Cecile Tiano alisema, vitu vilivyotolewa ambavyo ni pamoja na nguo, viatu,
kinga na pedi ni ishara ya upendo na hali ya kujali kwa kampuni na wafanyakazi
wa Tigo kutoa msaada kwa jamii ya watu wasiojiweza katika kipindi hiki cha
sikukuu ya Pasaka.
"Pia
tumetambua umeme wa kudumu ni moja ya hitaji muhimu sana hapa shuleni ndiyo
maana Tigo imeahidi kulipa gharama zote za matumizi ya umeme ya hapa shuleni
kwa mwaka mmoja kupitia Tigo Pesa," alisema Bibi Tiano. Shule maalum ya
Sinza maalum inahudumia watoto 88 na vijana wenye umri wa miaka kati ya 9 na 25
ambao wanatoka katika familia zenye mazingira magumu au wanaoishi na mzazi moja
au wanaishi na wazee.
Meneja
mkuu alifuatana na wafanyakazi wa Tigo na wasanii watano wa Bongo flava akiwemo
msanii Fid Q,Menina, Christian Bella na Barnaba katika tukio ambalo lilikuwa la
kusisimua na kupendeza kutokana na burudani ya moja kwa moja iliyotolewa na
wanamuziki.
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw.Simon Milobo alitoa shukrani zake za
dhati kwa kampuni ya Tigo,” hii sio mara ya kwanza kwa kampuni ya Tigo
kutusaidia uwa wanakuja mara kwa mara kutusaidia tunawashukuru sana, naomba na
makampuni mengine yaweze kujitokeza na kuiga mfano wa Tigo” alisema.
Msanii Fid Q akicheza nyimbo maalum ya kituo cha watoto wenye ulemavu cha Sinza Maalum na Mwalimu wa kituo hicho, wakati wa hafla ya kukukabidhi vitu toka kwa Wafanyakazi wa Tigo kwa kituo hicho kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka. |
Vifaa
mbalimbali vilivyotolewa kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka kwa Kituo cha Sinza
Maalum toka kwa wanyakazi wa Tigo.
|
Msanii Christian Belle akionyesha watoto jinsi
ya kutumia upawa wa kuchotea chakula |
No comments:
Post a Comment