Wednesday, April 1, 2015

UMESKIA ZAWADI AMBAYO SIMBA WATAMPA MCHEZAJI BORA MWAKA HUU,SOMA HAPA

Uongozi wa Klabu ya Simba umepanga kumpa gari mchezaji bora wa klabu hiyo katika sherehe za Simba maarufu 'Simba Day' inayofanyika kila mwaka Agosti 8.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Rais wa Simba Evans Aveva alisema kuwa chini ya uongozi wake wameanzisha tuzo hizo kwa wachezaji wa Simba ili kuibua morali ya wachezaji na kuthamini mchango wao na hiyo imekuja baada ya klabu hiyo ya wekundu wa Msimbazi kuingia mkataba wa miaka mitano na Kampuni ya EAG ambao watakuwa na jukumu la kuiwezesha Simba kupata mapato kwa njia mbali mbali ikiwemo udhamini kutoka makampuni mbali mbali.
Aveva alisema pia mbali na kumpa gari mchezaji bora wa klabu hiyo pia kutakuwa na tuzo ya mchezaji bora anayechipukia, kiungo, mshambuliaji bora na mchezaji mwenye nidhamu.

"Mchezaji bora atapata gari, mchezaji bora chipukizi atapata Sh5 milioni waliosali watapata Sh2 milioni ikiwemo mwenye nidhamu.

Aveva alisema pia mbali na tuzo hizo pia watatoa tuzo ya mchezaji aliyetukuka 'All Fame' ambaye nae atapata kiasi hicho cha fedha na pia mbali na zawadi hizo wachezaji hao watapewa simu aina ya Huawei.

Mbali na tuzo hizo Aveva alisema pia Kampuni hiyo ya EAG itakuwa pia na jukumu la kuhakikisha Simba inafanikiwa mikakati yake ya kuongeza mapato, kukuza namba ya wanachama, kuongeza na kuwapa faida wanachama wa Simba kupitia huduma za Bima, kuongeza ari ya wachezaji Simba, kuwaenzi na kukumbuka wachezaji wa zamani.

"Lengo la utekelezaji wa mikakati hii ni kukuza ajira kutokana na biashara zitakazoanzishwa, tunaamini tukitumia bidhaa za Simba ambazo tunalenga kuzifikisha kila sehemu Tanzania na kutengeneza mfomo wenye lengo la kuuipatia mapato stahiki tofauti na sasa.


"Kupitia mkakati huu Simba itakuwa na uwezo wa kujenga uwanja wake na kuwa na vyanzo endelevu vya mapato vitakavyoiwezesha kuboresha kiwango cha timu na kuifanya iwe bora si Tanzania pekee bali Afrika nzima....: "Kwa timu yenye mamilioni ya washabiki hili si jambo lisilowezekana bali linalowezekana, ni jambo la kufurahisha na kuona uongozi wa Simba umetambua hili."alisema Aveva.

Naye mkurugenzi wa EAG Group Iman Kajura akizungumzia suala hilo alisema "Kupitia  mkataba huu nataka kuona Simba inapata mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa kuitafutia vyanzo vingi vya mapato, ili iache kutegemea mapato ya  mlangoni na ada za wanachama pekee."

Kajura alisema mipango yote ya kuendesha zoezi hilo anaipata kutoka klabu ya Arsenal ya England ambayo anafanya nayo kazi katika kukuza na kuingiza wabia wa biashara.
HABARI NA MICHUZI BLOG

No comments: