Mwenyekiti wa ACT wazalendo mama ANNA MGHWIRA akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimio ya kamati kuu ya ckama hicho iliyoketi jana |
Baada ya kufanya uchaguzi wa chama na uzinduzi wa
chama kwa mafanikio makubwa chama kipya cha ACT-wazalendo nchini tanzania leo
kimetangaza kuanza kuishambulia mikoa kadhaa nchini kwa lengo la kutangaza
azimio la arusha baada ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho kuamua kufanya
hivyo.
AkizUngumza na wanahabari mapema leo mwenyekiti wa
ACT wazalendo mama ANNA MGHWIRA amesema kuwa kamati kuu ya chama imeamua kuanza
ziara ya ambayo ni ziara ya kwanza na kupita katikia mikoa takribani kumi yenye
lengo la kutangaza azimio la arusha lililiuhishwa baada ya kupitishwa na vikoa
vya chama ambapo amesema kwa sasa azimio hilo lipo katika hatua ya kuchapishwa.
Ziara hiyo ambayo itawahusisha viongozi wakuu wa
chama itapita katika mikoa ya Ruvuma,njombe,iringa,morogoro,Dodoma ,singida,tabora,shinyanga,mwanza
na mara,ziara ambayo amesema kuwa inatarajiwa kuwa na mafanikio makubwa katika
chaka kutokana na mapokeo ya chama hicho kuwa ni makubwa kwa watanzania.
Aidha katika hatua nyingine chama hicho kimeungana na
vyama vya UKAWA pamoja nna wanaharakati mbalimbali ambao kwa pamoja wamekuwa
wakipinga mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya ambapo kamati kuu ya chama
hicho nayo imetangaza rasmi kuwahamasisha watanzania pamoja na wanachama wa
chama hicho kuipigia kura ya hapana katiba inayopendekezwa kutokana na kile
walichokiita ni ubatili wa mchakato mzima wa kupatikana kwa katiba hiyo.
No comments:
Post a Comment