Waziri wa ushirikiano
wa Africa mashariki mh HARISON MWAKYEMBE amekutana Uongozi wa
wakala wa forodha na uondoshaji shehena Tanzania(TAFFA),kwa
lengo la kukaa kwa pamoja na kujadili chamgamoto mbalimbali ambazo zinaikabili secta
hiyo katika nchi za Africa mashariki.
Akizungumza katika
,mkutano huo waziri mwakyembe amesema kuwa ameamua kukutana na wakala hao kutokana na mchango mkubwa walionao katika
kuinua uchumi wa nchi na amekuwa na mahusiano ya karibu na wakala hao tangu
akiwa waziri wa uchukuzi hadi sasa wizara ya Africa mashariki.
Waziri mwakyembe
amesema kuwa amekuwa akipokea kero nyingi za maswala ya uondoshwaji wa shehena
kutoka katika nchi za Africa mashariki na kuzitatua lakini ameshangaa kwanini Tanzania
wamekuwa wagumu kupeleka kero zao kwa waziri huyo jambo ambalo limemsukuma
kukutana na wadau kama hao ili kujua ni changamoto gani zinawakabili na jinsi
gani wanaweza kuzitatua kwa pamoja.
Waziri wa ushirikiano wa africa mashariki mh HARSON MWAKYEMBE akizngumza na Uongozi wa wakala wa forodha na uondoshaji shehena Tanzania(TAFFA) alipokutana nao ofisini kwake jana kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili katika shughuli zao |
Wakizungumza na waziri
huyo viongozi wa TAFFA wameonyesha kutokuwa na imani na mamlaka ya mapato Tanzania
TRA kwa kile walichokiita ukiritimba uliokithiri juu yao wanaofanyiwa na mamlaka
hayo ikiwemo dharau pamoja na
kutosikilizwa keri zao jambo ambalo waziri MWAKYEMBE amesikitishwa nalo na kuahidi
kulifanyia kazi mara moja
Aidha wakala hao
wamelalamikia mfumo mbovu wa utoaji wa leseni kwa ajili ya kufanya kazi zao
ambao kwa sasa leseni kwa wakala hao zimekuwa zikitolewa kwa mwaka mmoja jambo
ambalo wamedai ni kero kwao kwani wamekuwa wakitumia muda mwingi sana katika
kufwatilia leseni kuliko kufanya kazi za kampuni zao jambo ambalo pia waziri
mwakyembe ameahidi kulisimamia kwa kina kuhakikishakuwa miaka ya leseni ya kazi
zao inaongezwa ili kuwapa unafuu wao katika kufanya kazi zao.
Katika mkutano huo
baada ya kuonekana wazi kuwa wakala hao wana changamoto nyingi za kuzungumza
waziri MWAKYEMBE aliahirisha mkutano huo na kuahidi kuwakutanisha tena siku za
karibuni kujadili kwa kina changamoto zinazowakabili ambapo mkutano huo unatarajiwa
kujumuisha wadau wengine wengi akiwemo waziri wa fedha pamoja na wadau kutoka
mamlaka ya mapato Tanzania TRA.
No comments:
Post a Comment