BILAL AKIMBIZA MWIZI KIMYA KIMYA--NAYE ACHUKUA FORM YA URAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha mkoba wenye Fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, baada ya kukabidhiwa mkoba huo na Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni , Seif Khatib, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo, Juni 4, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha mkoba wenye Fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa Fomu hizo. Kulia ni Mzee wa Chama cha Mapinduzi, Ramadhan Suleiman Nzori. Picha na O
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, baada ya kuchukua fomu, leo Juni 4, 2015. Kulia ni Mzee wa Chama cha Mapinduzi, Ramadhan Suleiman Nzori. Picha na OMR
Baadhi ya wana CCM waliohudhuria Mkutano wa Makamu wa Rais Dkt. Bilal. alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisani moja ya fomu za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati alipofika Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo Juni 4, 2015 kwa ajili ya kuchukua fomu hizo. Kushoto ni Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni , Seif Khatib. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment