Monday, June 15, 2015

MWANAMUZIKI AINEA AJIPANGA KUACHIA NYIMBO MPYA

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya nchini(BONGO FLAVOUR)Kedimon Ainea amesema ameshakamilisha kurekodi wimbo wake mpya ujulikano kwa jina umebadilika ambao ameshirikiana na Mwanamuziki Dulayo.

Akizungumza na mtandao huu jana,Mwanamuziki huyo alisema kuwa wimbo wake huo wa umebadilika umeshakamilika na muda wowote kuanzia sasa atausambaza kwenye vituo mbali mbali  vya redio.


Alisema kuwa wimbo huo wa umebalika ameutunga maalumu ikiwa moja  ya kuwaelezea wanawake ambao wanakuiuka na kusahau ahadi walizonazo.

Wakati huo huo Mwanamuziki amempongeza mtayarishaji wa muziki nchini 'ECK PRODUCTION'kutokana na dahamira ya kutaka kufufua vipaji nchini.

"nampongeza sana Eck Production kufuatia kitendo cha kuamua kusadia vijana,naomba watayarishaji wengine waige mfano huo"alisema.

No comments: