Monday, June 15, 2015

NDUGAI AOMBWA KUMSAIDIA MSANII ALIYETUNGA NYIMBO YA KUISHUKURU SERIKALI


MWENYEKITI wa Klabu ya Iyegu Fc ya Mlali,wilayani Kongwa mkoani dodoma Brayton masisila amemuomba Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya


muungano Job Ndugai kumpa ushirikiano Mwanamuziki Christian Muzmamoyo.

Mwanamuziki Christian Muzmamoyo.
Hatua hiyo imekuja juzi,wakati alipokuwa akifanya mahojiano maalumu na mwandishi wa mtandao huu kuhusiana na dhamira ya mwanamuziki huyo kutunga wimbo wa  kumpongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Prof Jakaya Kikwete kwa kile alichofanya ndani ya utawala wake 

Akizungumza na Mwandishi wa gazeti hili juzi,Mwenyekiti huyo alisema kuwa anamuomba Naibu Spika kwakushirikiana na wabunge wenzake wa ccm kumpongeza mwanamuziki huyo aliyeipongeza serikali yao.


Alisema kuwa Chama cha m


apinduzi 'CCM' ndiye serikali tawala hivyo kuna haja ya wabunge wa chama hicho kwakushirikiana na bunge wampongeza mwanamuziki huyo aliyejotolea kumpongeza  Rais kwa mazuri aliyowafanyia.

Wakati huo huo Mwenyekiti huyo amewaomba wambunge wa chama hicho kumtumia Mwanamuziki huyo wakati wa kampeni zao za uchaguzi kwakuwa  anaipenda serikali ya chama tawala.

Pia amemshukurua Mwanamuziki kufuatia kitecho cha kutoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya 500,000 kwa klabu ya Iyegu Fc kwaajili ya kukuza soka nchini.

No comments: