Kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam Dhehebu la shea inthnasheriya Tanzania Shekh HEMED JALALA akizungumza wakati wa semina hiyo |
Waumini wa dini pamoja
na viongozi mbalmbali na viongozi wa kitaifa katikia nchi zote duniani
wametakiwa kuliangalia Taifa la palestina kwa jicho la tatu kutokana na
kutengwa na mataifa mengi huku wananchi wa taifa hilo wakiendelea kuteseka
kutokana na vita iliyodumu kwa muda mrefu sasa.
Hayo yamesemwa leo Jijini
Dar es salaam na kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam dhehebu la shea
inthnasheriya Tanzania Shekh HEMED JALALA wakati wa semina ya maimam na mashekh kuhusu
QUDS (PALESTINA) na matatizo wanayoyapata wananchi wa taifa la palestina na
mataifa mengine ya masharaki ya mbali ambayo yamekumbwa na machafuko makubwa
kipindi cha karibuni.
Baadhi ya picha za matukio mbalimbali kutoka katimka machafuko huko Palestina |
Amesema kuwa Taifa la
palestina ni Taifa ambalo lina mchanganyiko wa dini na madhehebu mbalimbali
hivyo wanaoumia katika dhuluma hizo ni watu wa dini zote huku akitanabaisha
kuwa kuna haja ya wakristo na waislam nchini na duniani kuungana kwa pamoja
kupinga kwa kasi kubwa dhuluma hizo wanazofanyiwa Taifa la palestina.
Viongozi mbalimbali wa Dini ya kiislam waliohudhuria semina hiyo |
Amesema kuwa Palestina
ni nembo ya dunia kwani ndio nchi yenye historia kubwa duniani,na ni alama ya
dini zote kwani ina mchanganyiko wa dini mbalimbali,huku akisema kuwa ndani ya
taifa la palestina dhuluma yoyote wanayofanyiwa wapelestina ni dhuluma kwa dini
zote wakristo pamoja na waislam.
Amesema kuwa kwa sasa
wajibu mkubwa wa viongozi wa kidini na wapinga dhuluma kote nchini ni
kuhakikisha kuwa wanaueleza ulimwengu juu ya kile ambacho kinatokea katika mataifa
hayo likiwemo taifa la palestina,na kuwaeleza watu juu ya umuhimu wa taifa la
palestina kwa dunia na historia yake kwa ujumla.
Nje ya semina hiyo |
Semina hiyo ambayo
imewakutanisha maimam pamoja mashekh mbalimbali imefanyika Jijini Dar es salaam
kwa kuandaliwa na (Tanzania ithnasheriya TIC pamoja na hawzar imam swadiq yani
chuo cha imam swadiq kilichopo kigogo post jijini Dar es salaam.
Akizumgumzia malengo ya
kufanyika kwa semina hiyo kiongozi mkuu wa
kiroho wa waislam dhehebu la shea inthnasheriya Tanzania shekh HEMED JALALA
amesema kuwa ni kuwakumbusha watanzania kuwa amani hii iliyopo nchini kwa sasa
wajue kuwa na taifa la palestina wanahitaji kuwa nayo lakini wanaikosa hivyo
watanzania waiangalie palestina kwa jicho la pekee na kuona ni jinsi gani
wanaweza kuwasaidia.
No comments:
Post a Comment