Tuesday, June 9, 2015

WAZIRI MEMBE APATA WADHAMINI ZAIDI YA 800 KATIKA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa pili kushoto) na mkewe Dorcas (kushoto) wakifuatilia kwa makini jinsi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Lindi, wakati wakitia saini fomu za  kumdhamini kwa ajili ya kuteuliwa kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, katika Ofisi ya CCM mkoani humo Juni 08.2015, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 300.

Sehemu ya umati wa  wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Lindi, waliofika kwenye Ofisi ya CCM mkoani humo Juni 08.2015, kwa ajili ya kutia saini fomu za  kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 300.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mtwara, waliofika kwenye Ofisi ya CCM Mtwara mjini Juni 08.2015, kwa ajili ya kutia saini fomu za kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500. Picha zote na John Badi

Katibu wa CCM Mtwara mjini, Modesta Mwaya akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia), fomu zilizotiwa saini na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mtwara mjini, waliofika kwenye Ofisi hizo Juni 08.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500.

Sehemu ya umati wa  wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mtwara, waliofika kwenye Ofisi ya CCM Mtwara mjini Juni 08.2015, kwa ajili ya kutia saini fomu za  kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Lindi, waliofika kwenye Ofisi ya CCM mkoani humo Juni 08.2015, kwa ajili ya kutia saini fomu za  kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 300.Picha zote na John Badi

No comments: