Monday, June 8, 2015

TIZAMA LOWASA ANAVYOIZUNGUKA TANZANIA AZOA WADHAMINI 3,000 GEITA, CHATO NAKO APATA WA KUTOSHA


Lowassa akiteremka kutoka ndani ya ndege, kwenye uwan ja mdogo wa mdege a mgodi wa Geita (GGM)


Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa,(katikati), akipungia mkono
maelfu ya wana CCM na wananchi wengine waliofika kwenye ofisi za CCM wilayani
Geita Juni 8, 2015, kwa nia ya kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba
kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 25, 2015;
(Picha zote na K-VIS MEDIA)
Wakazi wa wilaya ya Geita, wakiwa juu ya nyumba na juu ya mti (picha ya chini), ili
kumuona Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa,
alipowasili kwenye ofisi za CCM wilayani Geita, Juni 8, 2015
 kuomba wana CCM wamdhamini baada ya kuchukua
fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu
wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015
Umati wa wana CCM waliofika kumdhamini Lowassa, na ananchi wengine waliofika walau kumuona wakiwa wamefurika nje baada ya ukumbi wa mikutano ofisi ya CCM wilayani Geita “kutapika” 
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge a Monduli, Mh.
Edward Lowassa, akipokea fomu za udhamini za CCM baada ya ,kujazwa na
wananchama wa CCM wilaya ya Geita, kwenye ukumbi wa CCM wilayani humo Juni 8,
2015. Mheshimiwa Lowassa, amedhaminiwa na jumla ya wanachama 3,000 wilayuani
hapo
Waziri Mkuu a zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Losassa, akiwaaga wananchi na ana
CCM waliofika kumdhamini kwenye ofisi za CCM wilaya ya Chato Juni 8, 2015.
Lowassa, akiwapungia wana ccm waliofika kumdhamini baada ya kukabidhiwa fomu za udhamini zilizojazwa. Jumla ya wana CCM 3,000 walijitokeza kumdhamini
Wana CCM waliofurika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za chama hicho ilayani Geita, wakimshangilia Lowassa
Lowassa, akiondoka huku akiwa amezungukwa na umati wa watu nje ya ofisi za CCM wilayani Geita

No comments: