Pichani ni Mwenyekiti wa chama cha ADC Said Miraji akizungumza na waandishi wa Habari mda huu Jijini Dar es Salaam |
SIKU chache kupita baada ya Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa kukihama chama chake cha awali cha Mapinduzi CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,navyo vyama vingine vya upinzania vimekishukia Chadema na kusema kimeua upinzani nchini.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo jiijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha ADC Said Miraji wakati alipokuwa anazungumzia suala la Lowassa kuhamia Chadema ambapo tayari ameshachukua fomu ya Kugombani Urais kupitia Chadema. Chadema ambao umeunda Vyama vya upinzani vya kutetea katiba ya Wananchi UKAWA,ambapo Miradi amesema kwa sasa vyama vya upinzania vimejishusha hadhi kwa watanzania.
“Kitendo hiki kimezidi kudhihirisha kuwa vyama vya upinzani tunapozungumza vitu basi vinavyokuwa ni vya uongo,kwasababu Katibu mkuu wa chadema Dakta Slaa aliaminisha umma kwamba lowassa ni miongoni mwa mafisadi papa”
“Halafu leo wamemkaribisha kwenye chama chao na kumpa nafasi ya Urais,sasa leo watanzania watatuona sisi wapinzani ni waongo maana yale aliyoyasema Slaa pale mwembe yanga ni uwongo au?”amehoji Miraji.
Miraji ameongeza kuwa kitendo cha chadema kumsimisha lowassa kunazidi leta mpasuka kwa wananchama waliokijenga chama hicho kwa zaidi ya miaka 20.
“Inakuwaje mtu ahamie leo na leo hiyo apewe uongozi tena wa juu,maana ndani ya chama hicho kuna makada waliokijenga chadema toka 1992 lakini leo hao hao hawapewi nafasi ya kugombani urais badala yake leo unawatupa unampa mtu aliyekuja leo kisa anaumaarufu wa watu,je hivi unategemea wananchi wengine hawatakubali”ameongeza.
Aidha Miraji amekitahadharisha Chadema kuacha tabia ya kutegemea kuwachukua wabunge na madiwani kutoka CCM na kuwapa uongozi kwa kusema suala hilo litaweza kukivuruga chama hicho kwa madai ya kuwa CCM wamepandikiza watu wake kuja kumaliza upinzani nchini.