Kipindi cha Kiswahili cha BBC Televisheni Dira
ya Dunia sasa kinakujia na muonekano mpya unaovutia.
Kipindi hicho kinachopeperusha Taarifa ya
habari kwa zaidi ya wasikilizaji milioni 6.9 itakuwa na sura mpya inayojumuisha
maandishi mapya yaliyotiwa nakshi,vipindi vipya na ripoti za kina
zinazojumuisha habari, michezo na burudani.
Tangu ilipozinduliwa mwaka wa 2012 Dira ya
Dunia TV, inatazamwa kila siku na mashabiki nchini Tanzania, Kenya, Burundi na
katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Aidha ina mashabiki si haba katika
mitandao ya kijamii.
Mtangazaji nyota wa idhaa hii ya Kiswahili,
Salim Kikeke, alitunukiwa mataji ya Tuzo Za Watu na Mtangazaji bora wa Runinga
wa mwaka, kwa mwaka wa pili mtawalio.
Mshindi wa tuzo hizo anachaguliwa na umma.
Kikeke anasaidiana na watangazaji wenza,
Kassim Kayira, Zuhura Yunus na Peter Musembi.
Dira Ya Dunia yenye sura mpya itaendelea
kuwaletea wageni wenye uzoefu wa maswala tofauti.
Wageni waliohojiwa tayari katika Dira ya dunia
ni pamoja na rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, rais Pierre Nkurunziza wa Burundi
na rais Yoweri Museveni wa Uganda mbali na wasanii waliobobea kama vile Diamond
Platnumz kutoka Tanzania, Eddy Kenzo kutoka Uganda na Juliani wa Kenya.
“Siamimi kwa hakika kuwa imekuwa takriban
miaka mitatu tayari .
Imekuwa safari ya kuvutia sana.
Mapokezi yetu katika kanda zima ya Afrika
Mashariki na kati ni ya kufana na kuridhisha.
Tunapania kuendelea kuwapasha habari
wasikilizaji wetu kuwa elimisha na pia kuwa burudisha kwa miaka mingi.
Hii sura tunayoizindua ni thibitisho tosha
kuwa ari yetu ni hiyo.”, anasema mtangazaji nyota Salim Kikeke.
Kwa upande wake Mhariri na Mtayarishi mkuu wa
Dira ya Dunia bi Mariam Omar anasema kuwa ”inafurahisha mno kwa mtazamaji kuwa
tunaimarisha kipindi chetu maarufu ”Dira ya Dunia.”
Tutaendelea kuwapa watazamaji wetu habari za
utendeti zaidi na kwa njia za kuvutia watazamaji wetu ambao bila shaka watakuwa
na uwezo zaidi wa kuwasiliana nasi na kuchangia habari tutakazo peperusha.”
No comments:
Post a Comment