Na Mwandishi wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeliahirisha rasmi Baraza la Madiwani
ambapo mgeni rasmi katika kuahirisha Baraza hilo alikuwa mheshimiwa Rais mstaafu
wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi.
Shughuli hizo zilianza kwa kikao cha baraza cha kawaida cha
kupokea taarifa ya utekelezaji ambapo baada ya hapo aliwasili mgeni rasmi
Mheshimiwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na kufuatiwa na tukio la kupita
katika mabanda maalum yaliyoandaliwa yakionyesha shughuli za kila idara na
kupata maelezo ya shughuli zinazofanywa na idara hizo pasitisha moja na
mafanikio mbalimbali katika idara hizo.Baada ya mgeni rasmi kupita katika
mabanda hayo na kupata maelezo ndi[po kilianza kikao rasmi cha baraza cha
kusitisha rasmi baraza hilo ambapo lilianza kwa ufunguzi wa sala na kisha
utambulisho uliofanywa na Mstahiki Meya Yusuphu Mwenda kabla ya wawakilishi
mbalimbali wa vyama vya siasa kutoa neno.
Akiongea mkurugenzi wa jiji alilipongeza baraza la Madiwani
na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondonikwa kazi nzito waliyoifanya ambayo
Tanzania nzima wanaikubali ikiwepo ukusanyaji mzuri wa mapato na kumalizia kuwa
Manispaa hii ni mfano mzuri wa kuigwa na Mstahiki Meya ni Meya wamfano kwa
Tanzania nzima.Akiongea katika kikao hicho mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni
alilishukuru Baraza la madiwani kwa ushirikiano wao katika kutekeleza shughuli
za maendeleo kwa Manispaa hii ambapo ni mengi sana yaliyotekelezwa na mengine
kutokana na muda bado hayakuweza kutekelezeka,lakini ameahidi kuyatimiza yale
ambayo wameyabariki yafanyike likiwepo la kujengwa kwa mtambo wa kuchakata taka
huko mabwepande ambapo tayari na mkataba umeshasainiwa wa kuanza kujengwa kwa
mtambo huo kwa msaada wa Humburg city.
Mgeni rasmi alitoa medani na vyeti kwa madiwani na kwa
baadhi ya watendaji akiwepo Mkurugenzi.Katika kuitambulisha timu ya KMC-FC
ambayo ni timu ya Manispaa ya Kinondoni mgeni rasmi alikabidhiwa jezi ya timu
hiyo yenye jina lake Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ,hali kadhalika madiwani
pia walipewa jezi hizo kila mmoja zenye majina ya kila mmoja na mkurugenzi
aliwaomba kuitangaza timu hiyo na kuisaidia kwa hali na mali .
Akiongea katika hafla hiyo Mstahiki Meya aliwashukuru wakazi
wa kinondoni kwa ushirikano.kuhusiana na suala la maendeleo Meya alisema
kumekuwa na ushiriki mpana wa wananchi katika maendeleo na pia uboreshwaji wa
fedha za matumizi ya umma kwa kujenga mashule,barabara,mahospitali ambapo
aliiongelea pia hospitali ya Mabwepande ambayo itakuwa ni msaada mkubwa kwa
wananchi,akiongelea upande wa mapato alisema pato limeongezeka sana kutoka
bil.11 kutoka kipindi cha nyuma hadi kufikia bil.35 hivi sasa.Akiongelea suala
la vibali vya ujenzi kwa sasa vimekuwa vikitolewa na kupunguza msongamano na nia
ni kuhakikisha vibali vya ujenzi vinapatikana ndani ya wiki moja,kuhusu usafi.
alisema Manispaa imekuwa ikishinda mfululizo katika
mashindano ya usafi yanayosimamiwa na wizara ya afya pamoja na hilo aliongelea
pia mpango kabambe wa alioucha katika mchakato wa utunzaji wa coco beach ili
kuiboresha na kubadilishwa sura yake licha ya hayo manispaa hii pia imekuwa
ikipata tuzo ya kutunza mahesabu vizuri,.Pia alimshukuru Naibu Meya Songoro
Mnyonge kwa ushirikiano na ushauri mzuri ambao amekuwa akimpa na mkurugenzi kwa
ubunifu na ushirikiano wake pamoja na watendaji wote kwa ujumla.Kaimu mkuu wa
mkoa akiongea alipopewa nafasi alisema haihitaji hata maelezo kuelezea Manispaa
ya Kinondoni kwani juhudi zao zinaonekana kwa macho.Mgeni rasmi akiongea katika
hafla hiyo aliwashukuru kwa heshima hiyo waliyompa kwani alikuwa ana hamu kubwa
ya kuja kuonana na watendaji wa Manispaa hii ,alisifia kazi nzuri ya kuboresha
maendeleo katika Manispaa hii na kuongeza kuwa Kinondoni ina uwezo wa kuendesha
mambo vizuri kwa kuja kwake katika hafla hii amefundishika haswa.Hongera
Manispaa ya Kinondoni.
No comments:
Post a Comment