Kingunge amesema
"Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili
kuisadia Kamati Kuu ktk kuwajadili wagombea"
Amesema Kamati ya
Maadili ya safari hii imefanya kazi isiyowahusu kikatiba - kukata majina ya
wagombe.
Kingunge amesema Kamati
ya Maadili ya CCM yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za
chama.
Amesisitiza Kamati
ya Maadili haikuwa na madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo
ilipaswa kuhoji wagombea wote 38.
Kwa mujibu wa
Kingunge, Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati ya Maadili kuandaa watu
wao na kuwakata wengine kwa sababu zao. Kingunge amewapongeza sana kina
Kimbisa, Nchimbi na Sophia kukataa maamuzi ya Kamati Kuu, waliisamamia Katiba
ya Chama.
Kingunge anadai CCM
ni chama cha wanachama wote, taratibu na kanuni zikipuuzwa na kufanya vitu kwa
maamuzi ya kikundi fulani.
Kwa mujibu wa
Kingunge, kwenye vikao vya CCM Ulifanyika uhuni na dharau kwa wanachama
wengine. Wakubwa waliopewa madaraka wanaona hakuna lolote tunaloweza kufanya
ila mimi nitasema.
Kingunge
anasisitiza, Kilichofanyika Dodoma hakikuwa sawa, Kamati Kuu iliporwa kazi
yake, hii ni dharau kwa wanachama na wagombea wote.
Anasema Kamati Kuu
ya Taifa CCM, ipo chini ya Halmshauri Kuu ya Taifa yenye madaraka ya kujadili
mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu; na Halmshauri Kuu ina madaraka ya kukataa
au kukubali mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu, lakini utaratibu huo
haukuwepo.
"Nawaheshimu
sana Mzee Mkapa, Mwinyi, na Karume, lakini nasikitika waliotoa michango ya
kutotoa haki kwenye Kamati Kuu. Waliogombea 1995 walikuwa 16, Kamati Kuu
iliwasikiliza na kuandaa orodha ya watu 6," alisema Kingunge.
"Tulipofika
NEC - wajumbe wakasema mbona Jina La Lowassa halikuwemo, mjadala ulikuwa mgumu,
watu walisema lazima aingie kwenye orodha. Kwa mara ya kwanza muundo wa Chama
ulikuwa tested baada ya wajumbe kutaka jina la Lowassa kwenye orodha ya majina
6,” aliongeza Kingunge.
"Mimi na
Mwalimu tulishangaa kuona Lowassa anakubalika kiasi kile, Wajumbe wa Kamati Kuu
walikuwa kimya na kushindwa kutetea mapendekezo yao. Mwalimu na Mimi ikabidi
tuingilie kati na kusaida K'Kuu, tulifanikiwa kuwashawishi wajumbe wa NEC na
wagombea wakaanza kujieleza," aliendelea kuongeza.
Kingunge ameendelea
kudai kuwa, wote wakati huo walikubaliana kwamba NEC ina madaraka ya kukataa au
kukubali mapendekezo ya Kamati Kuu.
"Safari hii
tumeona wazi kwamba NEC yote msimamo wao ulikuwa wazi, lakini haikutumika
busara, vitu vikaenda kama vilivyopangwa na “KITENGO”. KITENGO kilitoa
maelekezo ya kumzuia Lowassa asipate haki yake ya msingi ndani ya Chama.
"Kuna watu
wananiuliza kwamba Lowassa Fisadi, na wewe mzee unamuunga mkono, sasa
ningependa kusema hivi:
"Hadithi ya
Lowassa kuwa ni fisadi haina mashiko, ilianza kwa kashfa ya Richmond. Kamati
Teule ya Bunge iliundwa na kutoa taarifa za ovyo sana, na hatimaye kwa kulinda
heshima ya serikali na chama akajiuzulu.
"Lowassa sio
kwanza kuwajibika kisiasa, ktk awamu ya kwanza ya Mwalimu - kuna viongozi wa
kisiasa waliuzulu. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
na Mkurugenzi wa Usalama Taifa wote walijiuzulu kisiasa na Mwalimu aliwashukuru
kwa kuwajibika.
"Lowassa
alijiuzulu kuwajibika kisiasa, lakini ikabadilishwa kuonekana ni yeye ndiye
aliyefanya makosa, ndio ukaanza wimbo wa ufisadi. Serikali yenyewe ilimsafisha
kupitia TAKUKURU, lakini wimbo wa ufisadi ukaendelea, wakaja na wimbo mwingine
wa Gamba.
"Yote haya
yalipangwa na 'KITENGO' kilichoandaa kashfa ya Richmond. Edward ana historia
ndefu ndani ya Chama.” aliendelea mzee Kingunge.
Kwa mujibu wa
Kingunge, Wilaya ya Monduli ni moja ya wilaya ambayo mambo ya Chama yanaenda
vizuri sana, na Kinana alimsifu Lowasa kwa hilo kuwa amekitumikia chama.
Kingunge anadai
Lowassa amekuwa mtendaji mzuri hata serikalini, kila sehemu aliyopitia
alionyesha namna alivyoweza kushughulikia matatizo ya wananchi.
Anadai mradi wa
maji wa Ziwa Victoria, walishindwa wakoloni lakini limewezekana chini yake
Lowassa akiwa waziri wa maji.
Amesema Lowassa
kila alipoenda amefanya vizuri, na huu mchakato huu wa juzi ndani ya CCM
umeonyesha wazi Lowassa anapendwa na watu.
"Zipo hadithi
za kijinga kwamba watu wanaojitokeza wamepewa pesa, ni mawazo ya watu
waliofilisika. Watu wanamlilia Lowassa hawamjui, hizo zote pesa zote anatoa
wapi? Ana kiwanda cha pesa - hata angekuwa Bakheresa asingeweza!” alisema mzee
Kingunge.
Mzee Kingunge
alisema Lowassa ana kila sifa ya kuwa Rais na mwenyekiti wa Chama, mwingine
yeyote inabidi ajifunze sana haya. Akasisitiza kuwa 'Uongozi wa Chama na Nchi
umetumia nguvu kubwa sana kupuuza wananchi wanataka nini na kuhakikisha
wanayempenda hapati kitu.
"Yalitokokea
Dodoma yametia doa kubwa ktk historia ya Chama chetu chenye kuheshimika sana
nje na nchi kiujumla. Nchi ili itengamae lazima chama kinachoongoza kijiendeshe
kwa misingi ya haki na demokrasia, yaliyojiri Dodoma yametia dosari kabisa.
Yaliyotokea Dodoma ni uvunjani wa misingi ya haki - wagombea walipaswa
kusikilizwa kwenye Kamati kuu, walivunjiwa heshima na kunyimwa haki…” alisema
mzee huyo.
"Chama kilichofanya
maamuzi ya Dodoma hakikuwa chama kinachozungumziwa kwenye Katiba. Nawaomba
viongozi wetu warudi kusoma ahadi za mwanachama, warudi pia wasome utangulizi
wa katiba ya CCM. Kilichotokea Dodoma hakikubaliki, si halali na si haki.”
alisema mkongwe huyo ndani ya CCM.
Kwa mujibu wa mzee
Kingunge, pamoja na haya yote lakini Chama lazima kiendelee. Amesema CCM
imempata mgombea, ndugu Magufuli, maneno yake ya leo hayamhusu yeye, yeye
hakuwepo ktk 'KITENGO' cha kuharibu mambo.
Mzee kingunge
ameongeza kuwa Lowassa yupo tayari kushirikiana na Chama kusaidia Chama kupata
ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu, lakini yaliyotokea lazima yazungumzwe
kwa uwazi ndani ya vikao vya Chama ili watu watoe madukufuku yao.
Kingunge anadai
Mkutano Mkuu umetamka Mgombea ni Magufuli, lakini ili kupata ushindi - chama
kitahitaji nguvu na ushirikiano wa ndugu Lowassa na kuongeza kuwa anaamini
Ndugu Magufuli atafurahia suala hilo na ataandaa mazingira mazuri ya kuipata
sapoti hiyo.
Anadai Kabla ya
Uchaguzi inabidi CCM kufanya mazungumzo ili wakubaliane na kukosoana lakini
mwisho wa siku watoke tukiwa wamoja ili kupambana na adui.
Mzee huyo amedai
Lowassa pia aliwashinda wote waliomtaka kuvua gamba na akaendelea kubaki ndani
ya Chama.
Kingunge ameulizwa
wakati wa Richmond alikuwa mbunge lakini hakuonekana kumtetea Lowassa, kwanini?
Amedai 'Vitu vingine havipaswi kusema hadharani, niliona mambo yameharibika,
nikakaa na Lowassa nikamshauri awajibike kisiasa.’
Ameulizwa kama ana
mpango wa kurudisha kadi ya Chama kuonyesha kutokuridhishwa na uvunjifu wa
katiba ya Chama; akajibu 'Siku nikitaka kurudisha kadi yangu nitawaambia, mimi
kadi yangu namba 8 na nilihusika ktk kuunda chama hiki, nikifikia maamuzi
nitasema.’
Mwisho amemalizia
kwa kusisitiza: “Yaliyotokea Dodoma si halali na si haki…”
Asanten
CREDIT JAMII FORUM TANZANIA
No comments:
Post a Comment