Jeshi la polisi nchini Tanzania
leo limetangaza kupata mafanikio makubwa katika operation maalum inayoendelea
ya kuwasaka watu waliohusika katika shambulio la kuvamia kituo cha polisi cha
stakshari jijini Dar es salaam na kuendesha mauaji ya askari wanne wa kituo
hicho pamoja na raia waliokua katika kituo hicho huku wakipora kiasi kun]kubwa
cha silaha na kutokomea kusikojulikana.
Akizungumza na
wanahabari muda huu jijini Dare s salaam kamishna wa polisi wa kanda maalum ya
Dar es salaam SULEMAN KOVA amesema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na
wananchi wema wamefanukiwa kukamata bunduki 16 huku 14 zikiwa ni zile zilizoibiwa
katika tukio la kituo cha staki shari na mbili zikiwa bado hazijulikani
ziliporwa kwa watu gani,
Amesema kuwa zoezi la
kuwasaka watuhumiwa hao lilianza mara baada ya kutokea kwa tukio la stakishari ambapo ilipofika tarehe
17 mwezi huu majambazi hao walijipanga kufanya tukio myinginme maeneo ya
mbagala jijini Dar es salaam ambapo wananchi walitoa taarifa kwa jeshi la
polisi na wakajipanga tayari kuwakabili.
Hili ndio sanduku lililokua limehifadhi pesa taslimu million 170 na kufukiwa chini huko mkuranga |
Amesema kuwa baada ya
kufika eneo la Twangoma mbagala polisi walijipanga kuwakabili na baadae majambazi
hao walitokea na kuanza kushambuliana na askari hao ambapo katika mapamano hayo
majambazi watano walikamatwa ambapo watatu kati yao walikuwa tayari wameshakufa
na wawili wapo hai hadi leo
Katika taarifa nyingine
ambazo jeshi la polisi kanda maalum ya dare s salaam walizipata jana tarehe
19 ni kuwa kulikuwa na taarifa kutoka
kwa wananchi kuwa kuna tetesi kuwa silaha zilizoibiwa kituo cha stakishari
zilikuwa zimefichwa katika maeneo ya mkuranga.
Jeshi la polisi
waliweka kambi katika maeneo hayo na kuanza msako maalum wa kuzisaka mahali
ambapo silaha hizo zilikuwa zimefichwa
ambapo katika tukio la kushangaza
lilionekana eneo ambalo lilikuwa limewekwa kinyesi cha binadamu na polisi
kupatilia mashaka na ndipo walipoamua kupachimba na kufanikiwa kupata silaha
hizo.
Baada ya kuchimba
maeneo hayo jeshi la polisi lilifanikiwa kukuta silaha aina ambazo ni bunduku
aina ya 16 ambazo 14 ni za stakishari,na risasi 55 huku risasi 28 ni zile zilizoibiwa katika
tukio la stakishari.
Pamoja na silaha hizo
jeshi hilo lilikuta sanduku kubwa lililokuwa na hela kiasi cha shilingi million
sabini ambazo hazikujulikana mara moja zilikuwa na lengo gani huku KOVA akisema
kuwa uchunguzi zaidi unaendelea.
Aidha kamishna kova
amesema kuwa pamoja na mafanikio hayo yaliyopatikana katika operation hiyo bado
jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam linaendelea na kazi kubwa ya
kuwasaka wahalifu hao kwa kuwa bado kuna silaha nyingi ambazo ziliporwa katika
tukio la stakishari na bado hazijapatikana.
TAARIFA ZAIDI NTAZIDI KUKUPA BAADAE
No comments:
Post a Comment