Sunday, July 5, 2015

WAZIRI CHIKAWE AZINDUA DUKA LA DUTY FREE SHOP GEREZA LA LILUNGA HUKO MTWARA

 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe akipanda mti baada ya kuzindua duka la 'Duty Free Shop' gereza la Lilungu mkoani Mtwara,kuia ni Kamishna Jenerali wa Magereza,John Minja akifuatiwa na Mkuu wa magereza mkoa wa Mtwara, Mussa Kaswaka ikiwa ni mwendelezo wa maafisa na askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kusogezewa huduma za kupatiwa bidhaa muhimu katika maeneo na mazingira yao kwa gharama nafuu kwa lengo la kuwapunguzia ukali wa maisha.(Picha na Haika Kimaro)

Kamishna Jenerali wa Magereza,John Minja akimwagilia maji mti aloupanda katika duka la bei nafuu 'Duty Free Shop' Gerezala Lilungu mkoani Mtwara ikiwa ni mwendelezo wa maafisa na askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kusogezewa huduma za kupatiwa bidhaa muhimu katika maeneo na mazingira yao kwa gharama nafuu kwa lengo la kuwapunguzia ukali wa maisha.(Picha na Haika Kimaro)

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe amewataka maafisa na maaskari magereza kuanza kujijengea nyumba za kuishi na kuachana na mambo ya anasa kabla ya kustaafu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la vitu mbalimbali vya bei nafuu,alisema kuwa ili kuwasaidia askari kufanikisha hilo wameendelea na adhma ya serikili ya kuwasogezea huduma ya maduka ya vifaa vya bei rahisi ‘Duty Free Shop’ katika gereza la Lilungu mkoani Mtwara ambalo litakuwa likiuza vifaa kwa bei nafuu ambavyo vitawapa askari fursa ya kujiandalia makazi mapema kabla ya kustaafu.

Alisema askari kuandaa makazi wakati ameshastaafu ni ngumu sana na kuwa ni busara kwa askari hao wakatumia fursa kupata huduma za bidhaa zinazohusiana na ujenzi zinazoatikana kwa bei nafuu kwaajili ya kujijengea makazi yao mapema ili watakapostaafu wasianze kuhangaika.

“Mtu kuanza kuandaa makazi wakati umeshastaafu ni ngumu sana,nitoe rahi kwa maafisa na askari magereza kuwa ni busara watakatumia nafasi hii ili kupata huduma za bei nafuu kwa kujijengea makazi yao mapema kusudi watakapostaafu wasihangaike na badala ya kuanza kununua vitu vya anasa,”alisema Chikawe

Hata hivyo alisema  kuwa serikali iliidhinisha utaratibu wa maafisa na askari wa majeshi ya ulinzi na usalama kusogezewa huduma za kupatiwa bidhaa muhimu katika maeneo na mazingira yao kwa gharama nafuu kwa lengo la kuwapunguzia ukali wa maisha na kwamba hilo ni duka la nane kuzinduliwa rasmi.

Akizungumza Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja alisema kuwa maafisa na askari wa magereza na wengineo wanapaswa kuzingatia masharti na kanuni mbalimbali zilizopo na zitakazotolewa kuhusiana na utaratibu wa kupatiwa huduma na kuwa hivi karibuni wanatarajia kufungua maduka mengine katika mkoa wa Arusha na Tanga.

“Naomba kuhakikisha kwamba mkataba wa uendeshaji wa huduma husika unatekelezwa kama ulivyoridhiwa na mwanasheria mkuu wa serikali na pandezote mbili kuukubali,Lakisema Jenerali Minja na kuongeza:

“Kwa upande wa jeshi la magereza tunaendelea kutekeleza azma ya serikali kwani tayari maduka yamefunguliwa Ukonga, Keko, Dodoma ,Kilimanjaro, Morogoro, Mwanza,Mbeya ,Tabora na Mtwara.

Akizungumza Stafu Sajenti, Msiagile Edwin alisema uwepo wa duka hilo utatoa fursa kwao kupata huduma kwa ukaribu na kuweza kutunza kiasi cha pesa tofauti na walivyokuwa wakiuziwa vitu vya bei ghali katika maduka ya mitaani.

“Tunashukuru serikali kwa kutujali na kutuletea duka la vitu vya bei nafuu kwani zamani tulikuwa tukitumia gharama kweda mbali kutafuta bidhaa amabzo sasa hivi tutazipata kwa ukaribu na kuhifadhi kiasi cha pesa ambazo zilikuwa zikizidi katika maduka mengine,”alisema Sajenti Edwin

Mwisho……

No comments: