Ikiwa ni siku chache Tangu
Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh BENJAMIN MKAPA
kutoa kauli ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi kuwa ni lugha
chafu, sakata hilo limeanza kuchukua sura mpya baada ya wadau mbalimbali kuanza
kujitokeza kulaani na kupinga matumizi ya lugha kama hizo katika kampeni za
uchaguzi wa mwaka huu.
Mtandao wa asasi za
kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO wamekuwa wa kwanza kuibuka
na kulaani vikali vitendo hivyo ambavyo wamedai kama tume ya uchaguzi na vyombo
husika vitafumbia macho vinaweza kusababisha machafuko na chuki kwa watanzania.
Akizngumza na
wanahabari leo Jijini Dar es salaam HELLEN KIJO BISIMBA kwa niaba ya
nmwenyekiti wa TACCEO amesema kuwa matumizi ya lugha za kejeli,dharau,na
vijembe katika kampeni yataleta chuki na hatimaye kupelekea uvunjifu wa amani
jambo ambalo lazima wanasiasa wawe makini wanapokuwa majukwaani kuepuka
kuwagawa watanzania na kuwapandikiza chuki.
Baadhi ya wanabari wakichukua Taarifa hiyo |
Akitolea mfano kauli aliyoitoa
Mh MKAPA katika viwanja vya jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama cha
mapinduzi siku ya jumapili ambapo alisema kuwa watanzania ambao wanataka
ukombozi wa Tanzania huku wakijua kuwa nchi tayari ilishakombolewa miaka mingi
iliyopita ni upumbavu na ulofa wa watanzania hao.Bi BISIMBA amesema kuwa kauli
kama hizo hazikutakiwa kutolewa mbele ya watanzania wenye mawazo na mihemuko ya
kisiasa na ilitakiwa lugha hizo kukemewa mara moja na mamlaka husika lakini cha
kushangaza hakuna mtu aliyejitokeza kulaani vitendo hivyo.
Aidha akizungumzia mambo
yanayoendelea katika mitaa mbalimbali ya kuzomea watu wenye sare ya chama
tofauti na itikadi zao TACCEO wamesema kuwa tabia hiyo kama ikiachwa bila
kukemewa kwa lugha moja inaweza kuhatarisha amani ya Tanzania katika kipindi
hiki cha uchaguzi mkuu kwani inajenga hasira kwa wale wanaofanyiwa vitendo hivyo
na baadae kuamua kufanya fujo.
Mtandao huo ambao leo
ulikuwa unatoa Taarifa kuhusu uhakikiki wa majina katika daftari la kudumu la
mpiga kura na mwenendo wa kampeni za uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani
wameelezea mambo kadhaa waliyoyabaini katika mazoezi hayo.
Katika zoezi la uhakiki
wa Daftari la kudumu la wapiga kura wamesema kuwa mchakato huo umegubikwa na
kasoro kadhaa ambazo wamezitaja kuwa ni kukosekana kwa taarifa sahihi za zoezi
zima la uhakiki wa majina ya waliojiandikisha,kukosekana kwa majina kwa baadhi
ya wananchi waliojiandikisha,majina kuonekana sehemu tofauti na ile
waliyojiandikisha pamoja na changamoto nyingi ambazo wameitaka tume ya uchaguzi
kuhakikisha kuwa wanazitizama mara moja kabla ya uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment