Chama cha ACT wazelendo
leo kimenza mafunzo ya siku mbili mfululizo kwa wagombea wake wa nafasi za
ubunge nchini mafunzo ambayo yamelenga kuwajengea uwezo na kujiamini zaidi kuelekea
kufanya kampeni na kutafuta nafasi za uwakilishi wa katika majimbo mbalimbali
kikiwa ni chama pekee nchini Tanzania kulichoendesha mafunzo kama hayo kwa
sasa.
Kiongozi mkuu wa chama
hicho ZITTO ZUBER KABWE akizungumza na wanahabari wakati wa mafunzo hayo amesema
kuwa chama hicho ni chama pekee nchini Tanzania kilichodiriki kuwapa mafunzo ya
kuelekea katika uchaguzi ili kuwaweka katika mstaari mmoja wa kuhakikisha kuwa
wanakwenda na lugha moja kwa watanzania kueleza mipango na ilani ya chama
hicho.
ZITTO KABWE akiendelea kutoa mafunzo kwa wagombea ubunge zaidi ya 90 walioshiriki katika mafunzo hayo |
ZITTO KABWE anasema
kuwa chama cha ACT wazalendo ndio chama pekee nchini Tanzania ambacho kina
agenda maalum kwa watanzania tofauti na vyama vingine ambavyo amesema kuwa
vinatumia mbwembwe na ulaghai kwa watanzania bila kuweka wazi nini wanataka
kuwafanyia watanzania.
Amesma kuwa mambo
ambayo chama hicho kimekuwa kikiyapigania na kitaendelea kuyapigania ni pamoja
na mambo ya hifadhi ya jamii kuhakikisha kuwa watanzania wote wanafaidika
nayo,pamoja na miiko ya uongozi na kukemea ufisadi kwa nguvu moja ambapo
amesema kuwa kwa sasa hakuna chama hata kimoja kinazubutu kusimama na kukemea
ufisadi kwani nao wamekuwa sehemu ya ufisadi huo.
HIZI NDIO HISTORIA
ZILIZOWEKWA NA ACT HADI SASA KUELEA UCHAGUZI MKUU.
Akizungumza Mh ZITTO
KABWE amesema kuwa kikiwa ni mara ya kwanza kushiriki katika uchaguzi mkuu
chama cha ACT WAZALENDO kimeweza kusimamisha wagombea ubunge katika majimbo 219
kati ya majimbo 265 jambo ambalo linakifanya chama hicho kuwa ni chama cha pili
kwa wagombea ubunge wengi huku cha kwanza kikiwa ni chama cha mapinduzi CCM.
Historia nyingine
ambayo chama hicho kimeiweka ni kuweza kusimamisha wagombea ubunge wanawake wengi
kuliko vyama vingine vyote nchini Tanzania ambapo chama hicho kimesimamisha
wanawake 25% sawa na wabunge 55 katika majimbo toifauti tofauti nchini Tanzania huku kubwa ni kusimamisha mgombea urais mwanamke.
Historia nyingine ni
hii chama cha ACT wazalendo ndio chama pekee kilichosimamisha wagombea wenye
umri mdogo kuliko vyama vyote nchini ambapo mgombea mwenye umri mdogo ana miaka
21 na mwingine akiwa na miaka 23 ambapo amesema kuwa ni ishara kuwa chama hicho
kinawajali vijana.
Mh ZITTO akizungumzia
changamoto ambazo chama hicho kinakumbana nazo amesema kuwa hujuma mbalimbali
kutoka kwa wapinzani wao zimekuwa nyingi ikiwemo kukatwa kwa majina kadhaa ya
wagombea wao bila sababu za msingi mfano jimbo la kinondoni ambalo msanii
KALAPINA alikatwa katika orodha ya wagombea bila kutolewa sababu jambo ambalo
limewafanya kukata rufaa.
Amesema kuwa hujuma
hizo sio mwaka huu zimeanza ni kila mwaka huwa zinatokea kutokana na vyama
vingine hususani chama cha mapinduzi kuishiwa na mbinu za ushindi na kuanza
kuwahujumu wapinzani,ambapo amesema kuwa wao kama ACT WAZALENDO wataendelea
kupigana hadi hatua ya mwisho.
Chama hicho kitazindua kampeni zake siku ya jumapili katika viwanja vya zakiem mbagala Jijini Dar es salaam ambapo wanataraji kuweka wazi mipango na ilani ya chama hicho.
No comments:
Post a Comment