Imeelezwa kuwa kama
viongozi wa dini na madhehebu yote nchini Tanzania wataamua kukaa meza moja na
kujadili pamoja na kushauriana njia za kuitunza amani ya nchi hususani kipindi
hiki kigumu kuelekea uchaguzi mkuu, hakuna mtanzania atakayeanzisha vuguvugu
lolote la uvunjifu wa amani kwani itasaidia watanzania kuaminiana kwa kila
mmoja na imani yake.
Kauli hiyo imeelezwa
leo jijini Dare s salaam na kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam dhehebu la shia
Ithnasheriya Tanzania SHEIKH HEMED JALALA wakati wa semina maalum iliyoandaliwa
na dhehebu hilo kwa wanahabari na wadau mbalimbali wa tasnia ya habari semina
iliyokuwa na lengo la kujadili kwa kina wajibu wa vyombo vya habari katika
kuelimisha jamii.
Sheikh JALALA amesema
kumekuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani nchini Tanzania huku akivitaja kuwa
ni pamoja na chuki baina ya waumini wa dini tofauti tofauti ambapo watu
wamekuwa wakikashfu dini za wengine,migogoro ya ardhi,mauaji ya watu wenye
ulemavu wa ngozi,dhuluma na ukandamizaji dhidi ya wanawake,pamoja na migogoro
kati ya wakulima na wafugaji.
Akizungumza na
wanahabari mbalimbali ambao walipata nafasi ya kuhudhuria semina hiyo amesema
kuwa huu ni wakati wa wanahabari kuwa makini na habari wanazotoa kwa watanzania
kwani wao ndio wameshikilia amani ya nchi kwa kutumia kalamu zao, hivyo lazima
wanahabari wahakikishe kuwa wanatoa habari ambazo zinawaunganisha watanzania na
sio kutoa habari ambazo zinaweza kuwagawa watanzania na mwisho kusababisha
machafuko yasiyokuwa na faida kwao

No comments:
Post a Comment