TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasikitika kuwepo kwa taarifa za uzushi ambazo
zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo
vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Habari hizi si za kweli
na tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais, hausiki
na taarifa hizo zilizoenea kwenye mitandao ya Kijamii na wala hajapanga tukio
lolote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia
msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Aidha tunatumia nafasi
hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa zisizo sahihi kwa
maslahi yao waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa kisheria. Tunawaomba
waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta taarifa sahihi kwenye
vyombo vinavyohusika na kutambulika.
Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa
Makamu wa Rais
10/8/2015
No comments:
Post a Comment